Benki ya Absa kuendelea kuwezesha hadithi za watoto kielimu - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, April 4, 2024

Benki ya Absa kuendelea kuwezesha hadithi za watoto kielimu

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere akizungumza katika hafla ambayo benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa watoto yatima wanaolelewa wa vituo vya Tuyata Orphanage Centre na Watoto Wetu Tanzania vilivyopo chini ya Taasisi ya Adonai El Roi Foundation jijini Dar es Salaam jana.

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

Benki ya Absa Tanzania imesema itaendelea kuweka kipaumbele katika kufanikisha ndoto za kielimu za watoto wa kitanzania katika kuboresha huduma za kibenki zinazohusu watoto, hususan akaunti yake maalumu ya watoto ya Absa Child Savings Account.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla waliyowaandalia watoto wenye uhitaji kutoka katika vituo vya watoto yatima vilivyo chini ya Taasisi ya Adonai El Roi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa, Bi. Ndabu Lilian Swere alisema hayo yanaenda kupitia lengo kuu la Benki Absa ambalo ni kuiwezesha Afrika na Tanzania ya Kesho Pamoja hatua Moja baadae ya nyingine kiuchumi sambamba na ahadi mpya ya Chapa yake isemayo ‘Story Yako ni ya Thamani’.

Watoto wana ndoto nyingi katika maisha yao, wapo wanaotamani kuwa madaktari, wanasheria, viongozi wa makampuni, viongozi wa kisiasa, tunathamini Story za watoto wetu, Absa tupo hapa kuwasapoti ili waweze kikamilisha ndoto za story zao.

Absa inatoa Huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali, ni kwa kutumia huduma hizi pia tunawezesha hadithi za wazazi ama walezi wa watoto hawa nao pia kuweza kikamilisha hadithi zao mbalimbali za kiuchumi.

Hii si mara ya kwanza kwa Absa kufanya shughuli za kujitolea kusaidia jamii, hivi karibuni tulisaidia watoto wanaozaliwa kabla ya siku zao, hawa pia tutaangalia ni namna gani nyingine bora zaidi ya kuwasaidia”, aliongeza Bi Ndabu.

Akizungumza kuhusu akaunti ya watoto ya benki hiyo, Mkuu wa Mkakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Heristraton Genesis alisema akaunti hiyo haina makato ya mwezi na anaweza kupokea riba hata mara mbili endapo hatatoa pesa zaidi ya mara moja katika kipindi cha miezi mitatu.

katika kuonyesha Benki ya Absa imejipanga vizuri katika kuziwezesha ndoto za watoto, tunatoa riba mara mbili katika kile kiasi kilichokaa ndani ya miezi mitatu Ili kuwarejeshea watoto waweze kukamilisha story za ndoto zao za kielimu.

Ni rahisi kufungua akaunti hii, mahitaji ni kitambulisho cha taifa cha mzazi ama mlezi, cheti cha kuzaliwa cha mtoto ama utambulisho wowote kutoka shule anakosoma mtoto, na akaunti inaweza kuendeshwa kwa kutumia huduma zetu za kidigitali bila kuhitajika kufika katika matawi ya benki”, alisema Bwana Genesis.

Naye Mwanzilishi wa asasi ya Adonai El Roi inayolea vituo mbalimbali vya watoto nchini, Bi. Ngole Melaisho alisema lengo lao kubwa la shirika lao lisilo la kiserikali pamoja na mambo mengine ni kutokomeza umasikini katika vituo hivi.

Taasisi yetu Ina malengo ya kuwafuatilia watoto hawa kwa umakini waweze kuendeleza ndoto zao kwa kupitia kukuza vipaji vilivyo ndani yao.

Nipende kuhamasisha watanzania waendelee kusaidia vituo hivi na pia kuongeza upendo kwa watoto hawa waweze kukamilisha malengo yao”, aliongeza Bi. Ngole.
Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa Benki ya Absa, Bwana Heristraton Genesis akizungumza katika hafla ambayo benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa watoto yatima wanaolelewa wa vituo vya Tuyata Orphanage Centre na Watoto Wetu Tanzania vilivyopo chini ya Taasisi ya Adonai El Roi Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (wa pili kulia) akikabidhi begi lenye vifaa vya shule kwa mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Johnson Helman katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi, Bwana Heristraton Genesis (kulia) na Meneja Kitengo cha Kadi wa benki hiyo, Elfrida Mruma wakishirikiana kutengeneza keki na watoto yatima wa vituo vya Tuyata Orphanage Centre na Watoto Wetu Tanzania vilivyopo chini ya Taasisi ya Adonai El Roi Foundation katika hafla ambayo benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa watoto hao jijini Dar es Salaam jana
Meneja Msaidizi wa Hoteli ya Johari Rotana, Ahmed Said (kulia) akikabidhi begi lenye vifaa vya shule kwa mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Abigael Maliki katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa kwa kushirikiana na hoteli hiyo kwa watoto wa vituo vya Watoto Wetu na Tuyata vilivyo chini ya Taasisi ya Adonai El ROI, jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya Absa Tanzania, Sandeep Chavda (kushoto), Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi, Bwana Heristraton Genesis, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum, Thereza Majinge na Meneja Kitengo cha Kadi wa benki hiyo, Elfrida Mruma wakipiga picha ya pamoja na watoto wa watoto yatima wa vituo vya Tuyata Orphanage Centre na Watoto Wetu Tanzania vilivyopo chini ya Taasisi ya Adonai El Roi Foundation baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya shule katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

  International forum poised to open up AFRICA - ASIAN economies to the world   By Peter Mgongo Dar es Salaam, Tanzania 29th April, 2024...

Pages