KAMPUNI YA ORYX TANZANIA NA ASAS WAGUSWA WATOA MSAADA WA VYAKULA NA MAJIKO YA GAS KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, April 14, 2024

KAMPUNI YA ORYX TANZANIA NA ASAS WAGUSWA WATOA MSAADA WA VYAKULA NA MAJIKO YA GAS KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

  

Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa (kulia), akipokea Moja ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Kampuni ya Oryx pamoja na Asas kwaajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea wilayani Rufiji mkoani Pwani kutoka Kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Shabani Fundi hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika Leo.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa (katikati), akipokea Moja ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Kampuni ya Oryx pamoja na Asas kwaajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea wilayani Rufiji mkoani Pwani kutoka Kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Shabani Fundi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika Leo. Kulia ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Asas Abdul Ally.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas Kwa kushirikiana na Kampuni ya ASAS wamekabidhi msaada wa vyakula pamoja na mitungi ya gesi ya oryx kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Msaada huo umekabidhiwa leo Aprili 13,2024 jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa.

Akizungumza wakati akipokea msaada huo Waziri Mchengerwa amesema kwa niaba ya wananchi  wanaushukuru kwa kupatiwa msaada huo unaokwenda kusaidia wananchi waliopatwa na mafuriko na kwa sasa wamehifadhiwa kambini kutokana na kukosa makazi pamoja na vyakula.

"Tunaashuhudia kuwepo kwa muamko wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye yeye ni mfariji namba moja katika Taifa letu alioutoa kwa siku ya jana alipokuwa kule Arusha lakini taarifa ambazo amekuwa akizitoa kuwataka Watanzania kuwa wamoja na kusaidia wale ambao wana nafasi basi wajitolee kwa ajili ya wenzao,"amesema.

Ameongeza kuwa hivyo leo wanashuhudia shehena ya vyakula ambavyo vimetolewa na ASAS pamoja na Kampuni ya Oryx Gas ambapo Oryx wametoa mitungi pamoja na majiko ambayo wananchi wa Rufiji hasa walioko makambini watakwenda kutumia.

Pia Oryx kwa kushirikiana na ASAS wametoa vyakula ambavyo vitakwenda kutolewa kwa wananchi wote walioko makambini ambao wanahifadhiwa na wanahudumiwa na Serikali kwa wakati huu huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia kwani tayari amekwisha elekeza  utolewaji wa shehena ya vyakula 

Ametaja vyakula hivyo ni  mchele  Maharage, unga pamoja naa vyakula  vingine ambavyo Rais Dk Samia ameelekeza kwenda Rufiji kwa ajili ya kusaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko kwa mwaka huu.

"Niendelee kuwasihi Watanzania wote katika maeneo yao wale wenye nafasi wanaona wanataka kutoa kwa ajili ya ndugu zao tunawakaribisha Rufiji.Nitume nafasi hii kuwashukuru na kuwaomba tuendelee kushikamana katika kipindi hiki kugumu, tuendelee kuwa wamoja na kwamba mafuriko hayo hayakuanza mwaka huu yamekuwepo tangu enzi wa baba wa Taifa."

Awali kabla ya kukabidhi msaada huo, Meneja Mauzo wa Oryx Gas Shaban Fundi  amesema kwa niaba ya  Oryx Energies wanatoa pole kwa waathirika wote wa mafuriko yaliyotokea nchini hususan watu wa Rufiji.

"Kampuni ya Oryx Gas ikishirikiana na wadau wenzetu ASAS tumeamua tuwashike mkono wenzetu wa Rufiji kwa kuwapa msaada wa vyakula na mitungi ya gas ili kusaidia watu waliopo katika makambi ya kutolea misaada ya kibinaadam.

"Tumetoa mchele, unga wa sembe, mafuta ya kupikia yenye thamani ya zaidi ya milioni 52. Zaidi tumetoa mitungi mikunwa 100 na majiko 100, pia tumetoa mitungi midogo 100 yenye thamani ya zaidi ya mili 25.Tunampa pole muheshimiwa Waziri Mchengerwa, Wananchi wa Rufiji na Serikali kwa ujumla,"amesema Fundi.

No comments:

Post a Comment

  International forum poised to open up AFRICA - ASIAN economies to the world   By Peter Mgongo Dar es Salaam, Tanzania 29th April, 2024...

Pages