ORYX: TUNADENI KUBWA KWA RAIS SAMIA, TUNAMUUNGA MKONO KUFIKISHA NISHATI SAFI - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Saturday, June 8, 2024

ORYX: TUNADENI KUBWA KWA RAIS SAMIA, TUNAMUUNGA MKONO KUFIKISHA NISHATI SAFI

Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas kama Benoit Araman (aliyeshika kipaza sauti) akisoma ujumbe uliondikwa katika Tuzo ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Kampuni hiyo kwa ajili ya kutambua mchango wa Rais katika Nishati Safi ya kupikia.Tuzo hiyo imepokelewa na Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson leo wakati wa Mashindano ya Siku ya Nishati Safi ya Kupikia Duniani ambapo kwa Tanzania Oryx wameshikiana na Wabunge wanawake kuadhimimisha siku hiyo


MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania, Benoit Araman amesema kuwa kampuni hiyo inaona, itambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matyumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi.


Amesema kuwa kwa kutambua mchango wa Rais Samia katika matumizi ya nishati safi wameamua kuungana na wabunge wanawake kumpa tuzo kumuunga mkono juhudi zake za kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.


Araman ameyasema hayo leo Juni 7, 2024 jijini Dodoma, katika Maadhimisho ya Siku ya Nishati Safi ya Kupikia Duniani ambapo Oryx, wabunge wanawake na wabunge vinara wa nishati safi walimtunuku tuzo Rais Dk. Samia kutambua mchango kuhamasisha nishati safi ya kupikia Tanzania na Afrika kwa ujumla.


Akitoa ahadi ya kampuni hiyo, amesema hadi sasa wameshatoa mitungi ya gesi na majiko yake 35,000 kwa makundi mbalimbali nchini na wataendelea na mkakati wao kwani dhamira yao ni kuona asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2032 inafikiwa kama ambavyo Rais Samia ameelekeza.


Benoit amesema tuzo hiyo ina ujumbe usemao “Kampuni ya Oryx Energies inatoa tuzo hii kwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutambua uongozi wake wa kipekee katika kushinda na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania na Afrika.”


Awali Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake nchini Shally Raymond, amesema wabunge wanawake pamoja na wabunge vinara wa nishati kwa kushirikiana na Oryx wameamua kutoa tuzo kwa Rais huku akitumia nafasi hiyo kupongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.


Akizungumza katika maadhimisho hayo Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson aliyekuwa mgeni rasmi, amesema kuna kila sababu kwa wabunge na Oryx kumpa tuzo Rais Dk. Samia kwa kuwa amekuwa kinara wa nishati safi ya kupikia na juhudi zake zinashuhudiwa na Watanzania, Afrika na dunia kwa ujumla.

Amesema Rais Samia alipokuwa nchini Dubai na hivi karibuni aliposhiriki mkutano kuhusu nishati safi ya kupikia Paris, Ufaransa ametambuliwa kuwa kinara wa nishati hiyo.


Hivyo wanaendelea kusisitiza Rais Samia ndiye kinara wa nishati safi ya kupikia.


Amesema katika Bara la Afrika kunachangamoto ya nishati ya kupikia na takwimu zinaonesha asilimia 80 ya wananchi barani humo wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia na kwamba kutoka katika nishati hiyo itachukua muda.


“Hivyo Rais Dk. Samia anasaidia kupunguza muda kwa kuendelea kutafuta fursa kubadilisha upikaji kwa kuacha kutumia nishati chafu na kuhamia katika nishati safi ya kupikia kama gesi.


“Juhudi hizo za Rais zimeanza Tanzania na takwimu nchini zinaonesha asilimia 90 ya wananchi hadi sasa wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia.


“Hivyo juhudi za Rais zinatusogeza angalau kutoka asilimia 90 na kusogea hadi 25 ili wawe wachache wanaotumia nishati chafu ya kupikia,” amesema.


Akifafanua zaidi Dk. Tulia amesema wanafahamu nishati isiyo safi ina madhara kwa binadamu na kwa nchini takwimu zinaonesha vifo takribani 33,000 hutokea kila mwaka kutokana na athari za kutumia nishati isiyofaa, hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...

Pages