Tuesday, July 9, 2024

TUNATAKA KUONA TAFORI ILIYOBORESHWA - WAZIRI KAIRUKI
Na Happiness Shayo - Morogoro
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ametoa rai kwa Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Mb) kutimiza wajibu wao kuhakikisha Taasisi hiyo inaboreka na hatimaye kuchangia katika mapato ya Taifa.
Ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji kazi, kusikiliza changamoto za Watumishi na kuzupatia ufumbuzi.
Amesema katika kufikia malengo ya Taasisi ni lazima wakawa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao huku Serikali ikifanyia kazi changamoto za bajeti, vitendea kazi na upungufu wa Watumishi wote zinazowakabili.
"Fuatilieni fursa za mafunzo ili kukuza utendaji kazi wenu na mjitoe kufanya kazi kwa bidii na msikate tamaa" amesisitiza.
Aidha amewataka Watumishi hao kujiwekea mipango mbadala ya kuiongezea Taasisi hiyo mapato kwa kuandika maandiko mbalimbali ya kuomba fedha katika Taasisi zinazotoa fedha hizo akitolea mfano wa Earth Fund na nyinginezo.
Tags
# LOCAL
Share This
Newer Article
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA KADI YA MALIPO YA KIMATAIFA YA POPOTE VISA CARD
Older Article
SHILOLE ALAMBA DUME APEWA UBALOZI NA KAMPUNI YA ORYX GAS TANZANIA
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025MWENYEKITI WA CCM MKOA TANGA ASISITIZA AMANI SHEREHE ZA EID ELFITR
Hassani MakeroMar 30, 2025
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Na Happiness Shayo - Morogoro Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ametoa rai kwa Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Mb) kutimiza wajibu wao kuhakikisha Taasisi hiyo inaboreka na hatimaye kuchangia ...
No comments:
Post a Comment