Tuesday, August 27, 2024
Home
BIASHARA
MAMA LISHE BABA LISHE MKOANI MBEYA WAMEINGIA KWENYE MTANANGE WA KUKATA NASHOKA MASHINDANO YA MAPISHI KWA KUTUMIA ORYX GAS
MAMA LISHE BABA LISHE MKOANI MBEYA WAMEINGIA KWENYE MTANANGE WA KUKATA NASHOKA MASHINDANO YA MAPISHI KWA KUTUMIA ORYX GAS
MAMA na BABA LISHE Wameingia kwenye mtanange mkubwa wakutafuta mpishi anaeweza kutumia gesi ya Kampuni ya Oryx Gas huku lengo la mashindano hayo ni kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kama ambavyo Rais Dk.Samia amedhamiria kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania iwe inatumia nishati hiyo.
Akizungumza na wana habari mkoani hapa leo Agosti 27,2024 jijini Mbeya , Meneja Miradi ya Nishati Safi kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema mashindano hayo yanatija kubwa kwa Mama Lishe na Baba Lishe kwani wanatambua kundi hilo ndilo linaloathirika kiafya kutokana na kutumia kuni na mkaa kwa muda mrefu.
"Mama baba Lishe anakaa muda mrefu anapokua anapopika kwa kutumia mkaa kwani tunaambiwa wananchi wengi wa Tanzania wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na matatizo ya kupumua au matatizo ambayo yanatokana na madhara ya kuni na mkaa.
"Sasa katika kundi hilo tunaweza kusema Mama na Baba Lishe ndio waathirika wakubwa , hivyo ni jamii ambayo sasa hivi sisi Oryx tunamkakati wa kuhamasisha iachane na matumizi ya Kuni na mkaa. na kuni na mkaa kwasababu wao ndio wanakaa jikoni muda mrefu katika kupika kila siku ndani ya siku 365,"amesema Ndomba.
Amesisitiza kwa hiyo Mama Lishe na Baba Lishe waanze kubadilika na kuanza kutumia nishati safi hivyo kutawasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na kuokoa maisha yao, mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kunalenga kuliepusha kundi hilo dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi ya kuni na mkaa.
"Lengo la mashindano haya ni katika muendelezo ambao Oryx tumeuanza muda mrefu wa kuhamasisha na kusaidia kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika mapishi.
Kwa hiyo ujumbe wetu kwa watu watumie gesi katika kupika mapishi.Tunaamini nishati safi ya kupikia ni suluhisho la changamoto nyingi hasa za kiafya,kimazingira na kiuchumi,"amefafanua.
Pia ameeleza Oryx wanaamini wanalojukumu la kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na ndio maana tumeleta mashindano haya katika eneo la wazi ili kila mtu aone faida ya matumizi ya nishati safi.
Kwa upande wao baadhi ya Mama na Baba Lishe wanaoshiriki mashindano hayo wamempongeza Mbunge wao Dk Tulia Akson pamoja na Oryx Gas kwa KUANDAA mashindano hayo ambayo yanakwenda kuongeza hamasa ya matumizi ya nishati safi katika shughuli zao za kupika.
Kwa upande wao baadhi ya Mama na Baba Lishe wanaoshiriki mashindano hayo wamempongeza Mbunge wao Dk Tulia Akson pamoja na Oryx Gas kwa kuratibu mashindano hayo ambayo yanakwenda kuongeza hamasa ya matumizi ya nishati safi katika shughuli zao za kupika.
Akizungumza kuhusu mashindano hayo
Mama Lishe aliejitambulisha Kwa jina la Yusra Ismail anayefanya shughuli zake za mama Lishe eneo la Sabasaba jijini Mbeya amesema mashindano hayo yanamanufaa makubwa kwao kwani wanapata elimu kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi lakini na matumizi salama ya nishati hiyo.
"Gesi ya Oryx imekuwa mstari wa mbele kutusaidia katika shughuli zetu za mapishi, tunafanya shughuli zetu kwa haraka," huku akieleza kutumia kuni na mkaa kunapoteza muda lakini pia wanaathirika kiafya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment