AKIBA COMMERCIAL BANK YAJIKITA KUTOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WAJASILIAMALI WADOGO NA WAKATI. - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Sunday, April 13, 2025

demo-image

AKIBA COMMERCIAL BANK YAJIKITA KUTOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WAJASILIAMALI WADOGO NA WAKATI.

download
Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi (kushoto), akiwa Kwenye kikao na wateja na wajasiriamali (SMEs) kutoka Kariakoo, katikati ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki, ili kujadili changamoto zao na kushirikiana mawazo kuhusu masuluhisho yanayoweza kukuza biashara zao hafla hiyo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya hiyo Bi Wesi Olivia.

download%20(1)
Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi (katikati), akiwabkatika picha ya pamoja wateja na wajasiriamali (SMEs) kutoka Kariakoo, katikati ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki, ili kujadili changamoto zao na kushirikiana mawazo kuhusu masuluhisho yanayoweza kukuza biashara zao


Mnamo tarehe 12/04/2025 Benki ya Akiba  ilifanya kikao na wateja wake na wajasiriamali (SMEs) kutoka Kariakoo, katikati ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki, ili kujadili changamoto zao na kushirikiana mawazo kuhusu masuluhisho yanayoweza kukuza biashara zao. Hii ni sehemu ya juhudi zetu za kuwa karibu na wateja na kutekeleza dhamira yetu ya kuwawezesha wajasiriamali na kuimarisha elimu ya fedha, alisema Bi. Dora Saria Mkuu wa Kitengo cha masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bwana Silvest Arumasi, alielezea furaha yake kwa kushirikiana moja kwa moja na wateja, akisema, "katika Benki yetu , tunaamini kwamba mafanikio ya wateja wetu ni mafanikio yetu. Tunajivunia sana kushirikiana na wajasiriamali wote nchini  katika  kusaidia  kukuza biashara zao kupitia elimu ya fedha, mikopo, na huduma za kidijitali."


Akizungumza katika tukio hilo, Bi. Wezi Olivia Mwazani, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya Akiba, alisisitiza umuhimu wa kujenga uhusiano ya kudumu na wateja kwa kutoa huduma za kifedha zinazolingana na mahitaji yao.


 "Tunafurahi kuwa na fursa ya kuzungumza na wateja wetu moja kwa moja, kuelewa changamoto zao na kutoa masuluhisho ya kifedha ambayo yatasaidia katika mafanikio yao ya muda mrefu."


Wateja waliokuwepo waliotoa  shukrani zao kwa juhudi hizo,  wakielezea jinsi fursa ya kushirikiana na Benki hiyo  ilivyo muhimu kwa ukuaji wa biashara zao. Wengi walielezea kuwa mpango huu wa elimu ya fedha na huduma za kidijitali utawawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi.


Bw. Silvest Arumasi, Mkurugenzi Mtendaji wa ACB aliwashukuru wateja kwa uaminifu wao na ushirikiano wa muda mrefu, akiongeza, "Tunapenda kuwashukuru wateja wetu wa Kariakoo na maeneo mengine kwa ushirikiano wao ikiwa ni pamoja na kutuchagua na kutuamini. Pamoja, tutaendelea kuleta mabadiliko katika sekta ya SMEs na kusaidia katika maendeleo endelevu ya kiuchumi."


Benki ya Akiba  inaendelea  kutoa huduma za kibenki zinazolenga mahitaji ya wateja na kusaidia ukuaji wa biashara za watu binafsi, SMEs pamoja na makampuni makubwa na taasisi mbalimbali  kupitia huduma zinazokidhi mahitaji yao  na matumizi ya teknolojia ya kidijitali.

No comments:

Post a Comment

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi (kushoto), akiwa Kwenye kikao na wateja na wajasiriamali (SMEs) kutoka Kariakoo, katikati ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki, ili kujadili changamoto zao na kushirikiana mawazo ...

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *