Friday, February 12, 2016
![](https://1.bp.blogspot.com/-7Kd9qaiRHuA/WaEtZyc70TI/AAAAAAAADsA/7WUYBVoY-UwwjdEP3kDFPvH9htN0dDKgQCLcBGAs/s1600/demo-image.jpg)
Timu ya Taifa ya Tenisi ya Walemavu yaelekea Kenya kushiriki michuano ya Kimataifa
Katibu Mkuu wa Chama cha Tenisi Tanzania
(TTA), Bw. William Kallaghe (kulia) akizungumza
katika hafla ambayo timu ya taifa ya mchezo wa tenisi ya walemavu (wheelchair
tennis) ilikabidhiwa bendera ili kuwaaga kwa ajili ya safari yao kwenda nchini Kenya
kushiriki michuano kadhaa ya kimataifa ya
mchezo huo nchini humo. Kushoto ni makamu katibu mkuu wa TTA, Bw. Joshua Mutale
na Ofisa Michezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (MBT), Bw. Benson Chacha. Hafla
hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw. Benson Chacha (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa
TTA, William Kallaghe na kulia ni ni mmoja wa makocha wa timu hiyo, Bw.Riziki Salum.
Ofisa Michezo wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Bw.Benson Chacha (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa nahodha wa
timu ya taifa ya mpira wa tenisi, Juma Mohamed katika hafla yakuwaaga
wachezaji hao jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya safari yao kwenda nchini Kenya
kushiriki michuano kadhaa ya kimataifa ya
mchezo huo nchini humo.
Ofisa Michezo wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Bw.Benson Chacha (kushoto) akimkabidhi cheti Latifa
Nassoro kwa kutambua mchango wa udhamini wa Tanzania Petroleum Service.
Katibu Mkuu wa Chama cha
Tenisi Tanzania (TTA), Bw. William Kallaghe (wa pili kulia) akimkabidhi cheti
cha shukrani Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw.Benson
Chacha kwa kutambua mchango wa baraza hiko katika maendeleo ya tenisi nchini. wengine
pichani ni baadhi ya wachezaji wa timu hiyo. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar
es Salaam leo.(Photos by Brian Peter Mgongo)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar
Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...
No comments:
Post a Comment