Tuesday, February 9, 2016
Benki ya NBC yazindua kampeni ya malengo
Mkuu wa Huduma za Rejareja za
Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi
kampeni ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto
ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na kulia ni Meneja wa kampeni
hiyo, Mtenya Cheya.
Mkuu wa Huduma za Rejareja za
Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi
wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa
za Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za
Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe (kushoto), akizungumza kuhusu faida
mbalimbali za mteja wa benki hiyo atakayeshiriki kampeni ya malengo ya NBC.
Kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow.
Kampeni ya malengo itadumu kwa
muda wa miezi mitatu kutoka Februari 4 mpaka Aprili 30 2016. Katika kipindi hicho
cha miezi mitatu ya kampeni,wateja wanaoweka fedha watafaidika na kiwango cha kuvutia cha riba na kuwa katika
nafasi kubwa ya kushinda gari mpya aina
ya Toyota Land Cruiser Prado kama linavooeneka pichani.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC wakipozi kwa picha wakati wa uzinduzi
wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam. Hii ni kampeni ya tatu ya kuwekeza kuzinduliwa
na NBC na kama ilivyo katika miaka mingi kampeni zote zimekuwa za mafanikio
makubwa katika suala zima la mrejesho na ufahamu wa wateja. Mwaka jana NBC
ilizindua kampeni ya kuwekeza iliyopewa jina la “Weka Upewe” ambayo ilishuhudia
NBC ikitoa zawadi kadhaa kwa wateja wao nchini kote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar
Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...
No comments:
Post a Comment