Tuesday, February 2, 2016
Benki ya NBC Kitengo cha Retail chawazawadia wafanyakazi wake bora
Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa NBC Bw.
Gaudence Shawa akimkabidhi cheti Bw. Nelson Moshi kwa kuwa mmoja wa wauzaji
bora wa NBC kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya Retail Council Awards,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wafanyakazi wa NBC idara ya huduma
reja reja za kibenki wakisherekea na mwenzao, Evance Luhimbo (Mwenye vazi la
Kimasai) kwa kuibuka Meneja Kanda bora wa Mwaka 2015 wakati wa hafla ya Retail
Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha ni (waliosimama
kutoka kushoto) Mkuu wa kitengo cha mikopo, Bw. Andrew Lyimo (kushoto), Mkuu wa
Mauzo, Bw. Mongateko Makongoro, Mkuu wa kusimamia hatari za uendeshaji Bw. Arnold
Mhally na Mkuu wa Huduma Reja Reja Za Kibenki Bw. Musa Jallow. Wengine kwa
mbele ni Bw. Andrew Massawe na Bi Jaqueline Sindano.
Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa NBC Bw.
Gaudence Shawa akimkabidhi cheti Bw. Methody Tryphone (kulia), kwa kuwa mmoja
wa wauzaji bora wa NBC kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya Retail Council Awards,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Uendelezaji
wa Biashara wa NBC Bw. Eddie Mhina.
Meneja Tawi la NBC Sea Cliff Bi. Mariam
Kombo (Kulia) akipokea tuzo ya Meneja Tawi Bora kutoka kwa Mkuu wa Idara ya
Uzingatiaji na Utekelezaji wa sheria za Fedha (compliance and regulatory
affairs) wa NBC, Bi.Sarah Laiser-Sumaye, kwenye hafla ya Retail Council Awards,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kaimu Mkuu wa Huduma za Digitali na
njia za huduma mbadala, wa NBC, Bi. Cynthia Ponera (wa pili kushoto), akipokea
Tuzo ya Mkuu wa Huduma Reja Reja za Kibenki kutoka kwa Mkuu wa Idara hiyo Bw.
Musa Jallow wakati wa hafla ya Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar
es Salaam hivi karibuni. Wengine kwenye picha ni Mkuu wa kitengo cha mikopo,
Bw. Andrew Lyimo (kushoto), Mkuu wa Mauzo, Bw. Mongateko Makongoro, Mkuu wa
Huduma za Kibenki Binafsi, Bi. Ashura Waziri, na Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa,
Bi.Tulibako Paiti.
Mkuu wa Idara ya Huduma Reja Reja za
Kibenki Bw. Musa Jallow, akimvisha Bw.Robert Kimaro vazi la kimasaai baada
kutangazwa kuwa miongoni mwa wauzaji Bora wa mwaka 2015 wakati wa hafla ya
Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine
kwenye picha ni Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NBC Bw. Eddie Mhina na
(kushoto) na Mkuu wa Mauzo wa NBC Bw. Mongateko Makongoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar
Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...
No comments:
Post a Comment