Friday, June 3, 2016
![](https://1.bp.blogspot.com/-7Kd9qaiRHuA/WaEtZyc70TI/AAAAAAAADsA/7WUYBVoY-UwwjdEP3kDFPvH9htN0dDKgQCLcBGAs/s1600/demo-image.jpg)
Mshindi wa kampeni ya malengo ya Benki ya NBC akabidhiwa gari lake
Mshindi wa
Kampeni ya akaunti
ya Malengo ya
Benki ya NBC, Erastus Mtui (wa pili kushoto), mkazi wa Jiji la Dar es Salaam akipokea ufunguo wa gari jipya aina
ya Toyota Prado lenye thamani ya Dola za Kimarekani 100,000 kutoka kwa Ofisa
Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya NBC Tanzania, James Kinyany (wa pili kulia)
alilojishindia katika kampeni hiyo illiyochukua muda wa miezi mitatu.
Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa
Huduma Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow na kushoto ni mke wa
Erastus, Violeth Mtui na watoto wao.
Mkuu wa
Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Neema Rose Singo akifanya
mahojiano na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Alisema kampeni
hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu ilikuwa na lengo la kuhamasisha
wateja wao kuwa na moyo wa kujiwekea akiba kufanikisha malengo yao.
Mshindi wa Kampeni ya Akaunti Malengo ya
Benki ya NBC, Erastus Mtui (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu pamoja na
familia yake ndani
ya gari lao mara baada ya
kukabidhiwa. Kushoto ni
mkewe, Violeth na watoto wao.
Mtoto wa mshindi huyo, Praise Erastus Mtui (katikati), akielezea furaha yake
baada ya baba yake kushinda zawadi ya gari.Pamoja naye ni wadogo zake.
Mshindi wa Kampeni ya Malengo ya Benki ya NBC, Erastus Mtui (kulia),
akipozi kwa picha pamoja familia yake karibu na gari lao muda mfupi baada ya
kukabidhiwa. Bwana Erasus mkazi wa Makongo jijini Dar es Salaam amewaomba
wateja wa benki hiyo kuendelea kutumia akaunti ya Malengo ya Benki ya NBC ili
kunufaika na faida mbalimbali zinazopatikana kupitia akaunti hiyo.
Maofisa wa
Benki ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa kampeni ya akaunti ya
Malengo ya benki hiyo pamoja na familia yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar
Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...
No comments:
Post a Comment