Friday, October 14, 2016
Mahafali ya Sekondari ya Sullivan Provost, Kibaha kwa Mathias yafana
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,
Rachel Mwalukasa (kushoto), akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule
hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias mkoani Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Shule, Alex Nicholaus,
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Dk Ellen Kalinga na Mhandisi wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya UDSM (COICT), Dk Suzan Lujara aliyekuwa
mgeni rasmi katika mahafali hayo
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Ellen Kalinga, (wa pili kulia) akimpongeza Mohamed Ibrahim, mmoja wa wanafunzi waliofanya
vizuri kimasomo na kujizolea tuzo mbalimbali wakati wa mahafali ya pili ya
kidato cha nne ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi
karibuni. Wengine kutoka Kulia ni Mhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
ya UDSM (COICT), Dk Suzan Lujara, Mkurugenzi Mtendaji wa Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa na Mkuu wa
shule hiyo, Alex Nicholaus.
Mhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (COICT), Dk Suzan Lujara (wa pili kulia) akikabidhi
cheti kwa Alvin Mgaya, mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari
ya wavulana ya Sullivan Provost wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo,
shuleni hapo Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi karibuni. Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Rachel Mwalukasa na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam Dk. Ellen Kalinga
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan
Provost, Rachel Mwalukasa (katikati), akimlisha keki mmoja wa wahitimu wa kidato
cha nne wa shule hiyo wakati wa mahafali yao ya pili shuleni hapo, Kibaha kwa
Mathias, Pwani hivi karibuni.
Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan
Provost wakipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja nja baadhi ya walimu, viongozi
wa shule na mgeni rasmi wakati wa mahafali yao shuleni hapo, Kihaba, Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa (katikati),
akimpongeza Mkuu wa shule hiyo Alex Nicholaus katika mahafali ya
pili ya kidato cha nne ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwani
hivi karibuni. Anayeangalia ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya wazazi wa shule
hiyo, Janeth Alexander. (Picha na Brian Peter Mgongo)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar
Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...
No comments:
Post a Comment