Zantel yatoa mbuzi kwa watoto yatima kusherehekea sikukuu ya idd. - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, September 8, 2016

Zantel yatoa mbuzi kwa watoto yatima kusherehekea sikukuu ya idd.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Benoit Janin kulia), akikabidhi mbuzi 12 kwa Kaimu Mufti, Sheikh Ally Ngeruko kwa niaba ya vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya idd el Adha. Makabidhiano yalifanyika katika ofisi za BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni watoto kutoka katika vituo hivyo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Benoit Janin (wa pili kulia), akikabidhi mbuzi 12 kwa vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam kwa uratibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ambapo Kaimu Mufti, Sheikh Ally Ngeruko (wa pili kushoto nyuma ya watoto), alipokea msaada huo kwa niaba ya vituo hivyo. Makabidhiano yalifanyika katika ofisi za BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam jana.  Kulia ni Meneja Biashara wateja wa Makampuni wa Zantel, Kasongo Faraji.
Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia) akigawa juisi kwa baadhi ya watoto yatima katika hafla hiyo.
Meneja Biashara  wateja wa Makampuni wa Zantel, Kasongo Faraji (kulia), akizungumza katika hafla hiyo ambayo Zantel ilikabidhi msaada wa  mbuzi 12 kwa Kaimu Mufti, Sheikh Ally Ngeruko kwa niaba ya vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya Idd el Haji
Baadhi ya wawakilishi wa vituo vya kulelea watoto yatima wakichukua mbuzi waliotolewa na Zantel.(Picha na Brian Peter Mgongo)

No comments:

Post a Comment

SERIKALI YASISITIZA UTAALAMU NA UBUNIFU KATIKA UNUNUZI NA UGAVI

Serikali imewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kuongeza ubunifu, uongozi bora na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ufani...

Pages