Friday, August 5, 2016
Benki ya Barclays yashinda tuzo ya Benki Bora nchini kutoa huduma za VISA CARD
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania,
Abdi Mohamed (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam juzi kuhusu tuzo waliyopewa na
kampuni ya VISA baada ya kuibuka washindi wa kuwa benki bora nchini katika
kuhamasisha wateja wake kutumia kadi ya VISA. Benki ya Barclays ilizindua
kampeni ya miezi mitatu inayowahamasisha wateja wake kufanya manunuzi kwa
kutumia kadi ya VISA hivyo kuondokana na madhara yanayoweza kujitokeza kwa
kutembea na fedha nyingi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja wa rejareja na
biashara ndogondogo, Kumaran Pather na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, wote
wa benki hiyo, Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania,
Abdi Mohamed (katikati) na Mkurugenzi wa Wateja wa rejareja na biashara ndogondogo,
Kumaran Pather wakionyesha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, tuzo
waliyopewa na kampuni ya VISA baada ya kuibuka washindi wa kuwa benki bora
nchini katika kuhamasisha wateja wake kutumia kadi ya VISA. Benki ya Barclays
ilizindua kampeni ya miezi mitatu inayowahamasisha wateja wake kufanya manunuzi
kwa kutumia kadi ya VISA hivyo kuondokana na madhara yanayoweza kujitokeza kwa
kutembea na fedha nyingi. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Aron Luhanga.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya Barclays Tanzania na wandishi wa habari wakihudhuria hafla
ambayo uongozi wa benki hiyo ulionyesha tuzo waliyopewa na VISA baada ya
kuibuka benki bora nchini kwa kuhamasisha matumizi ya kadi ya Visa.
Baadhi ya maofisa wa benki ya Barclays wakipozi kwa
picha na tuzo yao mbele ya waandishi wa habari.
(All photos by Brian Mgongo)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar
Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...
No comments:
Post a Comment