Jiji la Dar es Salaam kufungwa CCTV Camera - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Friday, August 18, 2017

Jiji la Dar es Salaam kufungwa CCTV Camera


Jeshi la Polisi nchini kwakushirikiana na nchi ya Korea Kusini lipo katika mpango wa kufunga kamera za usalama (CCTV Camera) katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam ili kupunguza vitendo vya uhalifu pamoja na kupunguza idadi ya Askari wanaofanya doria.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa maadhimisho ya siku ya urafiki kati ya Tanzania na Korea kusini ambayo imefanyika kwa kuwakutanisha baadhi ya Askari Polisi waliowahi kupata mafunzo ya Upelelezi katika nchi hiyo.

Aidha IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi litaendelea kutilia mkazo katika kuwapatia mafunzo wataalamu wake wanaoshughulika na uhalifu kwa njia ya mtandao ili kuendana na kasi ya wahalifu wa njia hiyo ambapo amewataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini wahalifu wanaotumia mitandao kufanya uhalifu wao.

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Song Geum-Young amesema kufungwa kwa kamera hizo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na uhalifu ambapo amesema nchini Korea Kusini Kamera zimesaidia sana kupambana na vitendo vya uhalifu.


Nchi ya Tanzania na Korea kusini zimekuwa na ushirikiano katika Nyanja mbalimbali ambapo kwa Uapnde wa Jeshi la Polisi kila mwaka Askari wawili wamekuwa wakienda kujifunza katika Jeshi la Polisi la Korea Kusini.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages