Monday, August 14, 2017

WAHARIRI WAPEWA SOMO KUHUSU UZALISHAJI SARUJI NA UBORA WAKE
Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya
Nje wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Bi. Mtanga Noor (kulia),
akiwapokea baadhi ya wahariri wa habari wakati wa ziara ya wahariri wa habari
za biashara na uchumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari
walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Pongwe, Tanga juzi kujionea shughuli
mbalimbali za uzalishaji saruji, mipango ya maendeleo na changamoto
zinazowakabili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Saruji Tanga (TCPLC), Reinhardt Swart (kulia, akizungumza wakati wa ziara
ya wahariri hao walipotembelea kiwandani hapo, Pongwe, Tanga juzi kujionea
shughuli za uzalishaji wa saruji na mipango ya maendeleo ya kampuni hiyo.
Mmoja ya waandishi wa habari mkoani
Tanga, Mngazija akijitambulisha wakati wa ziara hiyo.
Baadhi ya maofisa na wataalamu wa
Kampuni ya Saruji Tanga wakiwa tayari kutoa elimu kuhusu uzalishaji saruji na
kujibu maswali wakati wa ziara hiyo.
Meneja Usambazaji wa
TCPLC, Samuel Shoo (kulia), akitoa elimu kuhusu hatua mbalimbali za
uzalishaji saruji na ubora wake kwa wahariri hao.
Baadhi ya wahariri wa habari za
biashara na uchumi wakiwa katika chumba cha kuendeshea mitambo cha kampuni
hiyo.
Meneja Machimbo wa Kampuni ya Saruji
Tanga (TCPLC), Godwin Kamando (kulia), akitoa maelezo kuhusu shughuli za
uchimbaji mawe katika eneo la machimbo ya kampuni hiyo wakati wahariri wa
habari za biashara na uchumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini
walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Pongwe, Tanga juzi kujionea shughuli
za uzalishaji wa saruji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Airtel Tanzania Yawapa Walimu Mafunzo ya Ujuzi wa Kidijitali Kupitia Mpango wa SmartWASOMI
Mkurugenzi wa Machapisho na Utafiti kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Bw. Kwangu Zabron Masalu (Katikati), akizungumza jijini Dar es S...

No comments:
Post a Comment