Huduma mbalimbali zaboresha NBC ikiadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, October 24, 2017

Huduma mbalimbali zaboresha NBC ikiadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja

Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tawi la Samora wakipozi kwa picha ya pamoja wakiwa katika umbo la moyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu kwa wateja wao kipindi hii benki yao ikiendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja.
Mteja wa Benki ya NBC, Neema Xibona (kulia) akionyesha furaha mbele ya wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Samora, Dar es salaam ambapo sasa NBC inaendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Wafanyakazi hao wanatumia muda wao kuwa karibu na wateja kusikiliza maoni yao kuhusu huduma na changamoto wazipatazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda (kulia), akizungumza na mmoja wa wateja, Elias Kaaya alipofika katika tawi lake kupata huduma.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kichwele, Frank Mwanga (kushoto), akisalimiana na mmoja wa wateja waliofika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam kupata huduma ambapo pia alipata nafasi ya kutoa maoni yake kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tawi la Chang’ombe wakirusha maputo pamoja na wateja wao kusherehekea mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.

Meneja wa NBC Tawi la Samora, Faustina Maeda, akimkaribisha Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi (kulia) alipotembelea katika tawi hilo kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa kwa wateja na pia alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wateja.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages