Wednesday, February 14, 2018
BIL. 161.9 ZIMETUMIKA KUBORESHA VITUO VYA AFYA 170-MAJALIWA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa jengo la mama na mtoto lililojengwa katika hospital ya Amana (wa pili kutoka kushot ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, wengine ni viongozi mbalimbali waserikali pamoja na uongozi wa kampuni ya Amsons Group. uzinduzi huo umefanyika leo jijin Dar es Salaam.
Hili ndilo jengo la mama na mtoto lililozinduliwa leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Waziri Mkuu Kassi Majaliwa wakiwa wamewabeba watoto mapacha waliozaliwa katika hospital ya Amana jijini hapa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alipowasili katika hospital ya Amana kwaajili ya uzinduzi wa jengo la mama na mtoto uzinduzi huo umefanyika leo.
.............................
SERIKALI imesema itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini kwa kujenga vituo vya afya na zahanati, hospitali za rufaa pamoja na upatikanaji wa dawa lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma nzuri.
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokuwa akizindua Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Amana iliyopo Halimashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salama ambapo Wodi hiyo imejengwa kwa udhamini wa kampuni ya Amsons Group Limited, kwa thamani ya sh.bilioni 1.2.
Waziri Mkuu amesema dhamira ya serikali ni kuona wananchi wanapata huduma za afya kwa urahisi na kwa ukaribu mahali popote nchini na kusema kuwa serikali imedhamiria kujenga zahanati katika kila kijiji nchini, kujenga kituo cha afya katika kila kata ambapo kitakuwa kama kituo cha rufaa cha zahanati zote ndani ya kata.
“Tutahakikisha hospitali zote za mikoa zinaingizwa kuwa chini ya Wizara ya Afya ili ziratibiwe moja kwa moja na wizara,”amesema Majaliwa.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuzipandisha hadhi hospitali za Amana, Temeke na Mwananyamala ili ziwe za rufaa ili kusaidia upatikanaji wa huduma kwa ukaribu zaidi.
Amesema miundo mbinu ya Afya itaendelea kukarabatiwa ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vya kisasa katika hospitali za Mloganzila, jijini Dar es Salaam, Benjamin Mkapa , Dodoma na hospitali zote za kanda.
“Sula la afya ni moja ya mpango kipaumbele vya serikali. Tuko katika utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya afya, ambapo kutoka 6321 mwaka 2010 hadi vituo 7680 mwaka 2016 likiwa ni ongezeko la asilimia 6.9,”alisema Majaliwa.
Amesema Rais John Magufuli ametenga sh.bilioni 131 kuboresha vituo vya afya katika kata kwa kujenga wodi ya kinamama na chumba cha upasuaji kwa wajawazito wanaojifungua na kuongeza kuwa vituo hivyo vitakuwa na sehemu ya magonjwa ya kawaida , maabara na nyumba ya mtumishi.
Waziri Mkuu amesema Rais Dk. John Magufuli ametoa sh.bilioni bilioni 129 kwaajili ya kununua vifaa vya tiba ambapo kila kituo kitapata mgao wa sh.milini 280.
Pia amesema serikali ilitoa magari ya wagonjwa 70 na kuyagawa vijijini ambapo wanatarajia kuleta magari mengine 120, na imekusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa kuwa na bejeti inayo kidhi mahitaji.
“Tunatambua changamoto ya upungufu wa watumishi hasa baada ya kuondoa wafanyakazi hewa. Serikali itaendelea kuajiri wafanyakazi zaidi pamoja na kuboreasha mazingira ya utoaji huduma za afya nchini" Amesema Majaliwa.
Aidha ameipongeza kampuni ya Amsons Group kwa kujitolea kujenga wodi hiyo na kuahidi kusema serikali inathamini mchango wake na itaendelea kuipa ushirikiana kampuni hiyo.
Pia aliutaka uongoziwa hospitali ya Amana, kuanisha nyumba zinazoizunguka hospitali hiyo ili kuangalia upanuzi wake.
Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda, alisema kampuni ya Amsons Group mbali na ujenzi huo pia itajenga majengo mengine mawili katika hospitali za Temeke na Mwananyamala.
“Wodi hii linauwezo wa kuchukua wagonjwa zaidi ya 100 ni muhimu kwaajili ya wanawake ambao walikuwa wanapata taabu ya kulala chini au watatu katika kitanda kimoja baada ya kujifungua,”alisema Makonda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment