CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, February 28, 2018

CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO

Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi 18,2018 Madagascar.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine.

Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto, Maputo.

Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola.

No comments:

Post a Comment

SERIKALI YASISITIZA UTAALAMU NA UBUNIFU KATIKA UNUNUZI NA UGAVI

Serikali imewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kuongeza ubunifu, uongozi bora na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ufani...

Pages