Saturday, February 17, 2018
Mkazi wa Dar ajishindia Suzuki Carry 'Kirikuu' promosheni ya Zantel Jero Yako
Washindi wa zawadi mbalimbali wa
promosheni ya Jero Yako kutoka Zantel wakipozi kwa picha ya pamoja
na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Bw. Sherif El-Barbary ( katikati – mwenye t-shirt
nyeusi) pamoja na wafanyakazi wengine wa Zantel mjini Zanzibar hivi karibuni.
Mmoja wa shindi wa promosheni ya Jero Yako ya
Zantel Ibrahim Ambar Khamis akijaribu
zawadi yake ya boda boda mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Zantel mjini
Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (kulia), visiwani humo hivi karibuni.
Mmoja wa washindi wa Jero
Yako ya kampuni ya Zantel aliyejishindia baiskeli, Rashidi Abeid (kushoto),
akipongezwa na Ali Abdallah Ali kutoka Zantel katika hafla iliofanyika mjini
Zanzibar juzi.
Mfanyakazi wa Zantel visiwani Zanzibar, Nayrat
Zahor (kulia) akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa aina ya Moto C 4G toka Zantel kwa mshindi wa
Promosheni ya Jero Yako, Bilkiss yussufmia
daudi visiwani humo hivi karibuni
Mmoja
wa washindi wa Jero Yako ya kampuni ya Zantel aliyejishindia baiskeli, Wahida
Simai Ubwa (kushoto), akipongezwa na Shinuna Kassim wa Zantel katika
hafla iliofanyika mjini Zanzibar juzi.
Mfanyakazi wa Zantel mjini
Zanzibar, Mohamed Jaye (kulia), akikabidhi zawadi ya baiskeli kwa mmoja wa
washindi wa promosheni ya Jero Yako, Burhan Salum Mohamed katika hafla
iliyofanyika visiwani humo hivi karibuni.
Meneja Masoko wa Zantel
Tanzania, Rukia Mtingwa (kulia), akipiga simu kwa mshindi wa mwezi wa
promosheni ya Jero Yako ambapo mkazi wa jijini Dar es Salaam, Twaha Abdallah Seif
alijishindia gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘Kirikuu’. Katikati ni Meneja wa
Huduma na Bidhaa wa Zantel Rehema Tarimu na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein. Hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment