Watanzania waishio Marekani wachangia Ofisi za walimu Dar - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Friday, February 16, 2018

Watanzania waishio Marekani wachangia Ofisi za walimu Dar

Rc  Makonda(katika) akikata utepe na kuweza kupokea na kuona vifaa vya ofisi za walimu, vilivyopo kaika makontena Bandarini jijini dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa akifafanua jambo
 Makontena  20 yaliyobeba vifaa vya ofisi za walimu, vilivyotokea nchini marekani
 Baahi ya vifaa hivyo

Wanafunzi wa Shule ya Msingi kurasini wakishuhudia zoezi hilo


Rc Mkonda akizungumza na walimu,mafisa elimu kata,pamoja na wanafunzi waliofika kushuhudia samani hizo za vifaa vya ofisi za walimu . 

 Mhe. Makonda akikata utepe.

Picha ya pamoja
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo  amepokea makontena 20 kutoka kwa Watanzania wanaoishi Marekani yakiwa na vifaa mbalimbali vya samani za ofisi za walimu wa mkoa huo.

Akizungumza katika hafla hiyo,  iliyofanyika Kurasini Temeke jijini hapo Rc Makonda  amesema huu ni wakati wa kurudisha heshima ya walimu kwani wamekuwa wakisahaulika sana na kuwafanya wafanye kazi katika mazingira magumu jambo ambalo ni hatari kwani litapelekea kutofanya kazi kwa ueledi na kufanya wanafunzi washindwe kufanya vizuri.

 "Kama walimu wetu hawatakuwa na mazingira mazuri ,hata wakilipwa mshahara mkubwa kiasi ganii na utumishi yakiwa magumu hawawezi  kuwa na utulivu wa kutosha tulisahau kuwawekea mazingira mazuri walimu na tukasahau kuwa yeye anamajukumu makubwa ya kuahamisha matiriao kutoka kwenye kitabu kwenda kwa watoto huu ni wakati wa kuboresha mazingira ya walimu wetu "Amesema Rc Makonda.

Ameongeza kuwa yawapasa watumishi wote wa umma kumsaidia Raisi magufuli katika kuwasaidia wananchi hususani kwenye swala la elimu ili kuondoa changamoto mbalimbali kwa wananchi na siyo kusubiri rais ndo aje afanye au kutatua kwani kodi ni za wananchi zinatumika hivyo yapaswa kuwatumikia vyema.

"Lazima sisi wasaidizi wa  Mhe. Rais wetu  John Magufuli tujiongeze tusibaki kila kitu kumsubiri, baba wa watu tumsaidie kutatua changamoto hizi za wananchi,kwani kodi za wananchi zinatumika hivyo ni vyema tukatatua changamoto kama hizi"Amesema Makonda.

Pia amezitaka taasisi mbalimbali katika mkoa wa dar es salaam kuwapa kipaumbele waalimu hasa katika taasisi za kibenki walimu wapoenda kutaka huduma waweze kuwa mstari wa mbele kuhudumiwa.

Aidha amesema kuwa wadau waliochangia kununua samani hizo wamemtaka alipie gharama ya usafirishaji kutoka marekani hadi hapa ambapo ameweza kuleta makontena 20 kati ya 36 ambayo yana vifaa hivyo.


Makonda aliowaomba wadau wa mradi huo wasaidie kulipia gharama za usafirishaji wa samani hizo  na gharama zingine za ndani ili ziweze kupatikana na kutumiwa sehemu husika.  Wakati huohuo, Benki ya Walimu – Mwalimu Commercial Bank – imelipia baadhi ya makontena hayo.

Naye makamu mwenyekiti anayesimamia mradi huo,  Solomon Urio, amepongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa  za kutafuta wadau mbalimbali wa kuchangia shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali hususani sekta ya elimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amempongeza Rc makonda kwa jitihada zake  za kuona umuhimu wa mwalimu na kusema kuwa ameweza kutatua changamoto kubwa na kuwasidia walimu hawa amabao wanafanya kazi katika mazingira magum.

Kwa upande wao walimu pamoja na maafisa elimu wamesema Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,ni mfano wa kuigwa kwani ameweza kuwasaidia walimu kusafiri bure ,pamoja na kuwasaidia kuapata viwaanja kwa bei nafuu.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages