Thursday, February 15, 2018
UBALOZI WA CHINA WAMKUBALI RC MAKONDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akihutubia wanafunzi pamoja na walimu wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi wa ofisi 402 za walimu katika Shule ya Sekondari ya Makumbusho zinazojengwa kwa udhamini wa Ubalozi wa China nchini Tanzania uzinduzi huo umefanyika katika shule hiyo jijini hapa leo.
Balozi wa china nchi Tanzania, Wang Ke, akihutubia wanafunzi pamoja na walimu wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi wa ofisi 402 za walimu katika Shule ya Sekondari ya Makumbusho zinazojengwa kwa udhamini wa Ubalozi wa China nchini Tanzania uzinduzi huo umefanyika katika shule hiyo jijini hapa leo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo
Ubalozi wa China Nchini Tanzania umeguswa na kazi nzuri inayofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuboresha mazingira ya walimu na kuamua kumzawadia Majengo Matano ya kisasa kwaajili ya ofisi za walimu ambapo leo RC Makonda ameweka jiwe la Msingi kuashiria kuanza kwa Ujenzi huo kwenye Shule ya Sekondari Makumbusho pamoja na kukabidhi Ramani ya jengo.
Ujenzi wa Majengo hayo Matano ni matokeo ya RC Makonda kuwasilisha ombi la ujenzi wa ofisi za walimu kwa Balozi wa China nchini Tanzania na kwakuwa kazi anayofanya RC Makonda inaonekana Balozi huyo alipokea kwa mikono miwili ombi hilo.
yatajengwa kwenye Wilaya Tano za Mkoa wa Dar es salaam ambapo ndani yake zitakuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi, Ofisi ya walimu wote, ukumbi wa mikutano, chumba cha kuhifadhi mitihani, vifaa vya michezo, chumba cha muhasibu, chumba cha kubadili nguo, mapokezi, vyoo, bafu huku zikisheheni furniture za kutosha ikiwemo viti, meza, makabati na AC ambapo ujenzi wa jengo hilo unataraji kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.
RC Makonda amemshukuru Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke kwa ujenzi wa majengo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaenda kupunguza mateso ya walimu kufanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kufanya kazi *kwenye madarasa.
Amesema dhamira yake kuboresha mazingira ya walimu ni kuwawezesha kutoa elimu bora itakayowezesha Taifa kuwa na wataalamu wa kutosha.
Kwa upande wake Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke amesema kwa miezi mitatu aliyoishi hapa nchini tangu alipoteuliwa kuwa balozi ameshuhudia maendeleo makubwa aliyofanya RC Makonda hivyo wameona wasikae kimya kwenye jambo hilo linalolenga kuleta ukombozi wa uchumi kupitia elimu.
Nao walimu wa shule ya makumbusho wamemueleza RC Makonda kuwa awali walikuwa wakitumia madarasa manne ya wanafunzi hivyo ujenzi wa jengo hilo ni neema kwao kwakuwa madarasa hayo yatarejeshwa kwa wanafunzi.
Mchoro wa ramani ambayo ndio kutajengwa ofisi hizo
Baadhi ya walimu wakitoa burudani katika hafla hiyo
Wanafunzi wakimuimbia Rc Makonda Happy birthday baada yakutangaza kuwa leo ndio sikuyake ya kuzaliwa.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akipokea ramani ya mchoro ya ofisi hizo
Balozi wa china nchi Tanzania, Wang Ke, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi hizo (wanne kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na viongozi wengine katika sekta ya elimu.
Zoezi la uzinduzi likiendelea
Baadhi ya vingozi wa manispaa ya Kinondoni walio hudhuria katika uzinduzi wa ujenzi wa ofisi za walimu
Wana nchi wa kinondoni walihudhuria katika uzinduzi wa ujenzi wa ofis za walimu shule ya Secondari Makumbusho
Kikundi cha vijana wa SCOUT wakiwa katika uzinduzi huo waki wa tayari kutekeleza majukumu yao ya ulinzi katika eneo hilo
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni wakiwa katika kushuhudia kile amabacha wana kiita utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment