Katibu wa TAVITA Otieno Peter (katikati) Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Taasisi ya TASWIRA YA VIJANA TANZANIA (TAVITA) wamelaani vikali taarifa zote za Uchochezi na Uvunjifu wa Amani na baadhi ya matamko dhidi ya serikali ya awamu ya tano hali inayopelekea kuligawa taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katibu wa TAVITA Otione Peter amesema wao kama taasisi wanalaani taarifa zote zinazotolewa na baadhi ya watu kupitia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii jambo linalopelekea kuvunja amani ya nchi iliopo.
"Sisi kama Jukwaa Tunalaani kwa nguvu taarifa zote za uchochezi zinazofanywa na baadhi ya watu kupitia vyombo vya habari, magazeti,pamoja na mitandao ya kijamii na hata na baadhi ya matamko dhidi ya serikali ya awamu ya tano taarifa zote zinazochochea uvunjaji wa amani ya nchi" Amesema Peter.
Amesema kila mwananchi ana fursa ya kulitumikia taiga ili kuchochea kazi ya kuleta maendeleo ,lakini wapo wanaotumia muda mwingi kuchochea uvunjifu wa amani kitendo ambacho siyo sahihi ivyo amewataka watu watumie muda huo kuelimisha jamii.
"Viongozi wa dini asasi za kiraia na kisiasa wana wajibu mkubwa wa kuelimisha jamii juu ya madhara makubwa yanayoweza kutokea ikiwa nchi yetu itaingia kwenye machafuko kwani kazi kubwa ya Viongozi wa dini ni kuwalea waumini kiroho na kimwili pamoja na mambo yanayoweza kufanywa na wananchi yakaleta faida kwa taifa" Amesema Peter.
Aidha wametoa pongezi kwa Serikali iliyopo madarakani kwa juhudi zinazofanywa katika kuliletea taifa manufaa hususani Mhe .Rais John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa letu
Kwa upande wake mwenyekiti wa taasisi hiyo Shabani Amiri Mwanga amewataka wananchi kutilokubali taarifa zinazotolewa kwa ajili ya kuharibu taswira njema ya nchi kwani hawa wanaofanya hivyo wanataka kuvuruga amani ya nchi iliyopo.
"Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mawakala ambao wanatumia saa 24 kutoa taarifa za kupaka matope ili kuharibu taswira njema ya taifa letu" Amesema
Amesema taasisi ya Taswira ya Vijana Tanzania ipo tayari kupambana kwa hali yoyote na watu hawa wanaotaka kuchafua amani ya nchi na kwamba wapo tayari kuunga mkono juhudi za Rais Dr. John pombe Magufuli kwa maendeleo ya taifa.
No comments:
Post a Comment