Sunday, March 24, 2019

MBUNGE SOPHIA MWAKAGENDA ATWAA TUZO YA DUNIA
Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda - Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya (CHADEMA) ambaye pia ni Mwanaharakati wa siku nyingi wa Wanawake na Watoto amepewa tuzo ya heshima ya "A Woman of the decade in Public life" iliyotolewa katika Mkutano maalumu wa Woman Economic Forum unaofanyika New Delh India ulioanza tarehe 26 April na utamalizika tarehe 01 May 2018 na unaoshirikisha Wanawake zaidi ya 2000 kutoka pande mbalimbali za dunia wakiwemo Viongozi na wale walioonyesha mabadiliko chanya katika jamii.
Katika mkutano huo Mhe. Sophia pia alipata fursa ya kuongea na Wanawake hao kutoka pande zote za dunia na pia amekuwa mwanamke pekee kwa Afrika Mashariki kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo ni ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa wa muda mrefu katika kusaidia wanawake na watoto nchini Tanzania ikiwemo kielimu, kiafya na kiuchumi ikiwemo juhudi zake anazofanya katika kuwawezesha wanawake katika msaada wa kisheria na katika kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwasaidia vifaa vya kufanyia shughuli zao ikiwemo vyerehani na vifaa vingine.
Habari katika Picha na Anna Peter
Tags
# LOCAL
Share This
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025MWENYEKITI WA CCM MKOA TANGA ASISITIZA AMANI SHEREHE ZA EID ELFITR
Hassani MakeroMar 30, 2025
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda - Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya (CHADEMA) ambaye pia ni Mwanaharakati wa siku nyingi wa Wanawake na Watoto amepewa tuzo ya heshima ya "A Woman of the decade in Public life" iliyotolewa katika Mkutano maa...
No comments:
Post a Comment