Friday, July 27, 2018
AZANIA BANK YAWAKUMBUKA WASTAAFU
Mkurugenzi wa Azania Bank akizungumza na vyombo vya habari kwenye uzinduzi huo.
Mstaafu Hezron Kigondo akielezea faida alizozipata kupitia mkopo wa wastaafu.
Mstaafu Hezron Kigondo pamoja na Mkurugenzi wa Azania Bank Charles Itembe wakati wa Uzinduzi wa Wastaafu Akaunti.
Katika kuendelea kusogeza huduma zake kwa wananchi zaidi na kutoa masuluhisho ya kifedha, Benki ya Azania leo imezindua huduma mbili mpya maalumu kwa ajili ya wastaafu kutoka katika mashirika mbalimbali ya kiserikali na hata ya binafsi. Huduma hizi ni Akaunti maalumu ya wastaafu (Wastaafu Akaunti) ambayo pamoja na faida nyingine za kibenki akaunti hii haitakuwa na makato yoyote na watapata ATM kadi bure huduma nyingine ambayo Azania Bank imeiletea kwa wastaafu ni fursa ya kupata mikopo kuweza kujikimu na kuboresha maisha yao.
Akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa huduma hizi Mkurugenzi wa Bank ya Azania Bw. Charles Itembe alisema “Azania Bank inaendea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha inaendelea kukuza maisha ya watanzania wote kupitia huduma mbalimbali za kifedha inazozitoa. Leo Azania Bank inazindua rasmi Mikopo ya Wastaafu na pia uzinduzi wa kampeni yetu tuliyoibatiza jina la Bega kwa Bega”
Mikopo hii ya wastaafu inalenga wastaafu wote wanaopata pensheni kupitia mifuko ya jamii ambapo kupitia mikopo ya wataafu mteja ataweza kufanya marejesho kwa miezi 72 yaani miaka 6. Alielezea Zaidi Bw. Charles Itembe.
Mzee Haron L Kigondo ni mmoja wa wanufaika wa huduma hii mpya ya mikopo kwa wastaafu ambapo pamoja na kushuhudia yeye kuupata mkopo wake ndani ya wiki chache tu, alisema “Mikopo hii kweli inakwenda kutupa nafasi sisi Wastaafu kuweza kuendesha maisha yetu na hata kuendesha biashara wakati tukiwa bado tunaendelea kusubiri mafao yetu, Ninaishukuru sana Azania Bank kwa wazo hili kwani litakwenda kusaidia wastaafu wengi sana kuweza kuboresha maisha pamoja na biashara zao”.
Azania Bank kwa sasa ina matawi 17 ambapo ndani ya wiki 3 zijazo inategemea kuwa na matawi 19 baada ya kufungua matawi mapya Dodoma na Morogoro, pamoja na matawi haya Azania Bank inatoa huduma kupitia ATM zaidi ya 270 za Umoja Switch na hii kutoa fursa kwa mtu yoyote popote Tanzania kuweza kupata huduma za kibenki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment