Wednesday, October 24, 2018
NBC yapongezwa kwa kudhamini maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji mjini Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Albert Chalamila (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema
Kileo kutokana na udhamini wa benki hiyo katika maonyesho ya mifuko ya
uwezeshaji, programu na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) katika hafla ya ufungaji rasmi wa
maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya jana. Kushoto ni
Katibu Tawala wa mkoa huo, Mariam Mtunguja.
Mkuu wa Uhai wa Wateja wa NBC Tanzania,
Gaudence Shawa (kulia) akizungumza na Mshauri wa Kilimo na Huduma za Fedha
Vijijini wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Samora Lupalla
(katikati) huku Ofisa Habari wa mfuko huo, Victor Kyando akiangalia katika
hafla ya ufungaji rasmi wa maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe
mjini Mbeya jana. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, William
Kallaghe.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa
pili kushoto), akipewa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za kibenki zitolewa na
Benki ya NBC na Mkuu wa Kitengo cha Uhai
wa Wateja wa benki hiyo, Gaudence
Shawa wakati wa maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu na vikundi vya
kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC) na kumalizika juzi katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani Mbeya
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya, Jasmine Kilalile (kushoto), akitoa
ufafanuzi wa faida za kujiunga na huduma mpya ya NBC Kikundi Mobile kwa baadhi
ya wakazi wa Mbeya waliofika katika maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu
na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) na kumalizika juzi
katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment