Tuesday, November 13, 2018
Benki ya Biashara ya DCB yazindua uuzaji wa Hisa zake jijini Dar
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (kushoto), akizungumza katika hafla ambayo DCB ilizindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam jana.Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenbzi wa DCB, Prof. Lucian Msambichaka (wa tano kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa uuzaji hisa za benki hiyo kwa mwaka 2018 jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa na maofisa wengine wa benki hiyo. Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa (kulia), akikabidhi hundi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka baada ya kununua hisa za benki hiyo muda mfupi baada ya DCB kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa. Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.
Baadhi ya wafanyakazi wa DCB na waalikwa wengine wakihudhuria halfla hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa (kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka ofisini kwake Dar es Salaam jana wakati akinunua hisa za benki hiyo muda mfupi baada ya DCB kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018. Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment