Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika CBA Julius Konyani, wa pili (kushoto) akibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Promosheni iliyopewa jina la Shinda na M-PAWA. akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi rasmi wa Promosheni iliyopewa jina la Shinda na M-PAWA. Kushoto ni Meneja Masoko wa Vodacom, wengine ni maofisa wa benki hiyo na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha.
Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi rasmi wa Promosheni iliyopewa jina la Shinda na M-PAWA. Watatu (wapilikulia) Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika CBA Julius Konyani ambae amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Wengine ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Jehud Ngolo pamoja na Sophet Mafuru kutoka SMSRTCODES LTD hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Vodacom kwa kishirikiana na Benki ya Commercial Bank of Afrika (CBA) wametangaza rasmi kampeni ya shinda na M -pawa itakayowawezesha wateja kujishindia zawadi kemkem.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa benki ya CBA Julius Konyani amesema wateja watakaoweka amana, kukopa na kulipa kwa wakati ndani ya wiki 6 kuanzia Novemba 1 watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
Amesema kuwa wateja 200 watakaoweza kuweka Amana ndani ya wiki 6 ambao huweka amana katika akaunti zao za M-pawa watashinda mara mbili ya amana walizoweka.
Aidha amesema kuwa wateja 15 wanaokopa na kulipa kwa wakati watazawadiwa kiasi cha shilingi 100,000 ambapo kwa kipindi Cha wiki 6 jumla ya wateja 96 watanufaika na zawadi hizo.
Konyani amesema droo kubwa itakayochezeshwa mwishoni kabisa zitatolewa Jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 100 , ambapo ni pamoja na bajaji tano zitakazotolewa kwa wateja watano ambao hukopa na kulipa kwa wakati kupitia M-pawa na mteja wa jumla atapata zawadi nono ya shilingi milioni 10.
Kwa upande wake Meneja masoko wa kampuni ya Vodacom Noel Mazoya amesema kuwa wao Pamoja na washirika wao ambao ni benki ya CBA wataendelea kuleta karibu huduma za kijamii kwa mfumo wa kidigitali.
Amesema kuwa hadi sasa wamewafikia zaidi ya wateja milioni 7 ambao wanatumia huduma ya Mpawa katika kuweka faida na kukopa na kwa usalama zaidi.
Mazoya amesema kuwa wateja wa Vodacom waendelee kutumia huduma hiyo ili waweze kunufaika na zawadi zinazotolewa na kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment