Maonyesho ya ng'ombe bora wa maziwa yafana Dodoma - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, June 19, 2019

Maonyesho ya ng'ombe bora wa maziwa yafana Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa Fahali bora kutoka Mbozi, Mkoani Iringa, Abraham Mwalutende wakati wa maonesho ya  Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi.Wapili Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith na Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kushoto), akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima alipokwenda kufungua rasmi Maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (IRLI), Dk. Jimmy Smith.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akizungumza wakati wa maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi. Wengine kutoka kulia ni, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith; Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima na Msimamizi wa Mradi wa Utafiti wa Vinasaba vya Ng`ombe wa Maziwa kutoka Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk.Okeyo Mwai.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa ng`ombe bora wa maziwa kutoka Meru, Mkoani Arusha, Emmanuel Nanyaro wakati wa maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto), akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Ng’ombe bora wa maziwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) pamoja na wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Dodoma juzi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith (kushoto), akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Ng’ombe bora wa maziwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) pamoja na wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Dodoma juzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akipongezana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith wakati wa ufunguzi rasmi Maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma jana. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages