Tuesday, September 10, 2019
Benki ya NBC yaendelea kusogeza huduma karibu na wateja
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega (kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya huku Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya akiangalia katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Arusha hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro (wa pili kushoto), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Linley Kapya wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na benki ya NBC jijini Arusha juzi. Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya (wa pili kushoto) akishikana mikono na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Arusha hivi karibuni. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro na Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Linley Kapya (katikati) akizungumza na baadhi ya wateja katika hafla waliyowaandalia jijini Arusha hivi karibuni kwa lengo la kufahamiana na kupata mrejesho wa huduma wanazopewa na benki hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu y...
No comments:
Post a Comment