BRELA YATOA USAJILI WA MAKAMPUNI VIWANJANI PAPO HAPO GEITA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, September 20, 2020

BRELA YATOA USAJILI WA MAKAMPUNI VIWANJANI PAPO HAPO GEITA

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya Biashara wa Wakala wa usajili wa Makampuni (BRELA) Mainrad Rweyemamu (kulia) akimkabidhi Mfuko wenye zawadi mbalimbali kutoka kwenye Taasisi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi (kushoto) wakati wa ujumbe wa wakuu wa wilaya wa Mkoa wa Geita walipotembelea Banda la BRELA kwenye maonyesho ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili Mkoani Geita.
Ofisa Habari Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) Christina Njovu (kulia) akijadiliana jambo na Msaidizi wa usajili Mkuu wa Taasisi hiyo Hellen Mhina (kushoto) kwenye maonyesho ya Madini yanayoendelea Mjini Geita.
Msaidizi wa Usajili wa Wakala wa usajili wa Makampuni (BRELA) Walter Masamu (aliyesimama) akiwa na Ofisa kutoka kwenye Taasisi hiyo Athumani Makuka (aliyekaa) wakiwa kwenye majukumu ya kikazi ndani ya Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonyesho ya Madini Mkoani Geita.

Maofisa kutoka Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) wakiwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kikazi ndani ya Banda lao katika maonyesho ya Sekta ya Maidini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili Mjini Geita. (Wakwanza kushoto) ni Ofisa Leseni wa BRELA Robert Mashika, (katikati aliyesimama) ni Msaidizi wa usajili Mkuu wa BRELA Hellen Mhina, na (wakwanza kulia) ni Mtaalam wa mifumo ya Kompyuta Hillary Mwenda.

Na: Richard Mrusha – GEITA

WANANCHI wa mkoa wa Geita wameshauriwa kutembelea Banda la wakala wa usajili nchini BRELA ambapo kwasasa wapo mkoani humo kwenye maonyesho ya kimataifa ya teknolojia ya uwekezaji katika sekta ya madini ili kupata huduma mbalimbali za usajili.

Wito huo umetolewa na Wakala msajili mkuu msaidizi wa BRELA Hellen Mlima wakati Akizungumza na Waandishi wahabari nankuelezea kwanini wameshiriki maonyesho hayo.

Amesema kuwa wao Kama Brela wameshiriki maonyesho hayo kwa la kuwasogezea huduma karibu wananchi wa mkoa huo hivyo wanawaomba kufika kwenye banda lao kupata huduma.

"Tunaomba wakitokeze waje wasajili, wasikose nafasi hii muhimu na tutakuwa hapa hadi semptemba 27, wachangamkie fursa." amesema Hellen. 

Amesema moja ya shughuli ambayo wanaifanya hapo ni kuhuisha kampuni na.majina ya biashara mfanyabiashara kuhakiki taarifa zake kwa Njia ya mtandao.

Ameongeza kuwa usajili wa Kampuni kwasasa ni rahisi ambapo mtu anatakiwa awe na Tin namba, leseni ya biashara Katiba pamoja na kitambulisho cha Taifa NIDA na awe mtanzania.

Pia amefafanua kuwa kwa mgeni lazima awe na Hati ya kusafiria, katiba ya biashara, wamiliki na mtaji nakwamba zamani walikuwa wanatumia mifumo ya kizamani lakini kwasasa ni mtandao.

Akizungumzia gharama za usajili amesema inategemea na mtaji wa muhusika hivyo wananchi hususani wa mkoa wa Geita wameombwa kutembelea kwenye maonyesho ya sekta hiyo ya madini na hasa katika Banda la Brela na watu wanaendelea kujitokeza kwa ajili ya kusajili au kuhuisha taarifa zao.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages