Sunday, September 27, 2020
ZANZIBAR WAADHIMISHA SIKU YA AFYA NA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUTOA ELIMU KWA WANAFUNZI
Msaidizi mrajis Baraza la Maafisa wa afya Zanzibar Mohamed Khamis Ali akitoa maelezo juu ya umuhimu wa uwepo wa maafisa afya katika madhimisho ya siku ya Afya na Mazingira Duniani iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Dk. Ali Mohamed Shein Muembeshauri Mjini Zanzibar.
Afisa afya kutoka Baraza la Maafisa Afya Zanzibar Farhat Lahdad Mohamed akiwasilisa mada ya Virusi vya Corona katika hafla ya madhimisho ya siku ya Afya na Mazingira Duniani ambapo mabibi afya na mabwana afya wametoa elimu kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Lumumba.
Mwanafunzi wa kitato cha pili katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba Zakaria Khamis Hamad akiuliza swali kwa mtoa mada wakati wa utoaji elimu ya afya na mazingira katika hafla ya madhimisho ya siku ya Afya na Mazingira Duniani.
Mwanafunzi wa Afya na Mazingira Fatma Saleh Ali kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Lumumba njia sahihi ya kunawa mikono katika madhimisho ya siku ya Afya na Mazingira Duniani.
Picha ya pamoja ya Maafisa Afya kutoka Baraza la Maafisa Afya Zanzibar, wanafunzi wa SUZA wanaosoma Afya na Mazingira na wanafunzi wa kitato cha pili wa Skuli ya Sekondari ya Lumumba. (Picha na Makame Mshenga)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment