Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, ametembelea soko la Karume lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia Januari 16 jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika soko hilo, alikagua na kushuhudia athari mbalimbali zilizotokana na moto huo ambao umeathiri miundombinu mbalimbali ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kusababisha baadhi ya sehemu kukosa umeme.
Akizungumza mara baada ya kutembelea soko hilo Naibu Katibu Mkuu Mahimbali amesema kuwa kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea katika Mikoa ya Ilala na Temeke inaendelea ambapo mafundi tayari wapo katika maeneo hayo.
Moto huo ulianza majira ya saa 9 usiku ambapo jitihada za kuuzima moto huo zilifanyika ili kudhibiti moto usienee katika makazi ya wananchi lakini kutokana na miundombinu ya soko hilo kazi ya kuzima ilikuwa ngumu na kusababisha na kuteketea kwa soko lote.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (katikati) akimsiliza Meneja wa Tanesco Kanda ya Mashariki Dar es Saalam na Pwani, Keneth Boimanda (kulia) wakati alipotembelea soko la Karume na kukagua miundombinu ya TANESCO iliyoathirika na moto huo, Januari 16, 2022.
No comments:
Post a Comment