MHE.OTHMAN MASOUD AZINDUA MRADI WA MAJI MASINGINI - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, December 27, 2023

MHE.OTHMAN MASOUD AZINDUA MRADI WA MAJI MASINGINI

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman, Masoud Othman, akizungunza katika ufunguzi wa Mradi wa Maji Masingini wakati Mhe. Makamu alipofika Masingini magharib A Unguja kuzindua rasmi mradi huo leo tarehe 27.12.2023. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kushoto), akipokea zawadi kwa Meneja wa Mradi wa Maji Masingini kutoka Kampuni ya L&T ya nchini India wakati Mhe. Makamu alipofika Masingini kuzindua maradi huo leo tarehe 27.12.2023. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman ,Masoud Othman, akifungua pazia kuashiria ufungunzi rasmi wa Mradi wa Maji Masingini wakati Mhe. Makamu alipofika Masingini magharib A Unguja kuzindua rasmi mradi huo leo tarehe 27.12.2023. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba ili kuendelea kuwepo rasilimali ya maji ardhini hapa Zanzibar ni lazima kuchukuwa hatua na kutilia maanani suala la uhifadhi wa Mazingira, kupanda miti na kutunza uoto wa asili ulipo usipotee.

Mhe. Othman ameyasema hayo huko Masingini wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja alipofungua mradi wa Uimarishaji na Uhuishaji wa Mfumo wa Usamabazaji maji Zanzibar, ikiwa ni shamra shamra za sherehe za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Mhe. Othman amefahamisha kwamba kufanya hivyo ndio kuieneleza rasilimali hiyo iendelee kuwepo na kuwanufaisha wazanzibari na kwamba utunzaji wa mazingira ndio unaozalisha maji.

Amesema kwamba ni jukumu la kila mwananchi na viongozi katika ngazi mbali mbali kuutunza mradi huo kimazingira na kimiundombinu ili kuhakikisha kwamba mradi huo ni wa watu wote na kwafaida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Amefahamisha kwamba ulezi wa miradi ya aina hiyo ni ya watu wote na kwamba kila mmoja anawajibu wa kushirikiana kuulea ili uweze kuwa endelevu na kuwa na manufaa Zaidi kwa wananchi.

Mhe. Othman amesema kaatika kutilia mkazo suala utunzaji wa Mazingira serikali kupitia Ofisi yake itazindua mradi mkubwa wa upandaji miti katika visiwa vyote vya Unguja na Pemba jambo litakalohitaji ushiriki wa kila mwananchi na viongozi ili kufanikisha kurejesha Zanzibar kuwa ya kijani.

Mhe. Mhe. Makamu amewataka wananchi kuhakikisha kwamba wanalipa bili za maji kwa kuwa kufanya hivyo ndio kuiufanya miradi ya maji kuwa endelevu na kuendelea kuwanufaisha wananchi wa Zanzibar.

Aidha amesema kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelipa umuhimu mkubwa suala la maji kwa kufanya juhudi za kuhakikisha ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya aina mbali mbali mbali ya maji.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini, Joseph John Kilangi amewatahadharisha wananchi wanaoungiwa na watakaoungiwa maji na mita kuhakikisha kwamba hawazichezei ili kuziharibu.

Amesema kwamba jumla ya wananchi milioni moja na laki tano wataunganishwa kwenye mfumo wa kisasa wa 'smati mita' na kuwataka wananchi wote kuendelea kuitunza miundo mbinu sambamba na kuwa na subra wakati serikali ikiendelea na mipango ya kukamilisha malipo ya vipando kwa wananchi waliopitiwa na mradi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa ZAWA Dk. Salha Mohammed Kassim amesema kwamba mradi huo umegharimu dola za Marekani milioni 92.18 na utekelezaji wa mradi umenza Aprili 2020 ambao umegawanyika katika sehemu tatu za utekelezaji.

Aidha amesema kwamba skimu ya Masingini imejumuisha uchimbaji wa visima vinane vikubwa ambavyo vimekamilika na vina uwezo wa kuzalisha lita laki nane na tiisini elfu kwa saa (890,000lita/saa) ambao utawanufaisha wananchi wa shehia ya Masingini, Mtufaani, Mwera na Mwembe mchomeke ambapo kazi ya ulazaji wa mabomba imekamilika.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa yaendeleza udhamini wake Absa Dar City Marathon

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (wa pili kushoto) akionyesha fulana zitakazovaliwa siku ya mbio ...

Pages