Wednesday, December 27, 2023

MIRADI YA MAENDELEO YA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI YAONGEZEKA - ZANZIBAR
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleimana masoud Makame akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi Salum Vuai akiuliza maswali katika Mkutano na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleiman masoud Makame alipokua akizungumzia kuhusiana na Mafanikio na Changamoto za Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR)
Na Takdir Ali – Habari Maelezo, Zanzibar
WAZIRI wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleiman Massoud Makame amesema miradi ya maendeleo imeongozeka katika wizara hiyo kutoka miradi 10 ya maendeleo mwaka 2020 hadi kufikia 17 mwaka 2023.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akilezea makakati na mafanikio ya Wizara hiyo, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema miradi hiyo imejumuisha sekta mbalimbali ikiwemo Uvuvi, Mwani, Ufugaji, Viwanda vya kusarifu madagaa na mwani, masoko na madiko, uhifadhi wa Bahari na utafiti.
Ameeleza kuwa mafanikio hayo ya kimaendeleo yanaifffiisha Serikali katika shabaha za kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050, na Mpango wa Maendeleo ya Zanzibar (ZADEP).
Aidha amesema Serikali inaendelea kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwapatia elimu, ubunifu na zana za kujiongezea ajira katika maeneo yao.
Amefahamisha kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuwawezesha wakulima wa mwani na wafugaji wa mazao ya baharini 23,000 ambao zaidi ya asilimia 90 ni wanawake wa vijijini.
Mbali na hayo amesema, Usafirishaji wa mwani nje ya Nchi umeongezeka kutoka Tani 11,382 zenye thamani ya Tzs Bilioni 11.70 mwaka 2020 hadi kufikia Tani 12,563 zenye thamani ya Tzs Bilioni 12.581 kwa mwaka 2023.
Sambamba na hayo amesema maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni lazima yazingatie uhifadhi wa maliasili hivyo amewaomba Wananchi kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kuleteleza mikakati iliojipangia.
Mbali na hayo amesema Serikali imetilia mkazo utafiti na sayansi ya bahari ili kupata taarifa sahihi zinazoimarisha utekelezaji wa sera za Uchumi wa Buluu.
Tags
# LOCAL
Share This
Newer Article
MHE.OTHMAN MASOUD AZINDUA MRADI WA MAJI MASINGINI
Older Article
MHE.HEMED ABDULLA AFUNGUA KITUO CHA AFYA CHA UZI NA NG'AMBWA
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025MWENYEKITI WA CCM MKOA TANGA ASISITIZA AMANI SHEREHE ZA EID ELFITR
Hassani MakeroMar 30, 2025
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleimana masoud Makame akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.Mwandishi...
No comments:
Post a Comment