Sunday, June 30, 2024
Home
LOCAL
Mwenyekiti CCM Kibiti ataka umoja na ushirikiano kuelekea uchanguzi serikali za mitaa 2024
Mwenyekiti CCM Kibiti ataka umoja na ushirikiano kuelekea uchanguzi serikali za mitaa 2024
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Juma Kassim Ndaruke akifurahia jambo wakati wa kikao cha madiwani wa wilaya ya Kibiti pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kilichofanyika Kibiti mwishoni mwa wiki. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kutoa tathmini ya utendaji kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwa miaka mitano iliyopita huku pia wakitengeza mpango kazi wakati huu wa kuelekea kwenye uchanguzi wa serikali za mitaa 2024.
Kutumia mashindano ya Ndondo Cup kwenye kuhamashisha wananchi kushiriki uchanguzi serikali za mitaa mwaka huu.
Pwani, Kibiti Jumapili 30 Juni 2024
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Juma Kassim Ndaruke ametoa wito wa kushikiana na kujenga umoja dhabiti wakati huu wa kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa 2024 huku pia akiwataka Wenyeviti wa vitongoji na vijiji kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuzungumzia miradi na miundombiu yote inayotekelezwa na CCM kwa wananchi katika maeneo yao kwani inaonyesha ni jinsi ngani chama kimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kinatekeleza ilani yake.
Ndaruke amesema haya wakati wa kikao ambacho kimekutanisha madiwani wote wa wilaya ya Kibiti pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambacho kilikuwa na lengo la kutoa tathmini ya utendaji wa viongozi wa vijiji na vitongoji pamoja na kuweka mipango kazi wakati huu wa kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa 2024.
"Tumewaita mwenyeviti wa vitongoji na vijiji katika kuwatia moyo na kuwapongeza kwa kufanya kazi nzuri kwa miaka mitano iliyopita kwa weledi, na kuthamini mchango wenu katika kusimamia miradi" amesema Ndaruke
Ameongeza kuwa kulekea uchaguzi wa mwenyeviti wa serikali za mitaa 2024 katika wilaya kibiti atahakikisha uchaguzi huo unakuwa wa haki huku akisisitiza kuwa kila mwenye nia ya kugombea nafasi ajitokeze kushiriki.
"Uchaguzi hautakuwa na vitimbi wala vurugu yoyote na kwa yule ambaye amejiandaa kutuvurunga tutamvuruga yeye kabla hajatuvuruga" amesema Ndaruke
Pia ametoa rai kwa Wagombea wa nafasi za umwenyekiti wa vijijini na vitongoji pindi uchaguzi wa serikali za mitaa utakapo fanyika waweze kukubali matokeo ya kushinda na kushindwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kibiti Ramadhani Mpendu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mama Samia Suluhu kwa kuleta fedha nyingi za maendeleo katika wilaya ya Kibiti huku akisema kila kata ya wilaya ya Kibiti kwa sasa inayo shule za sekondari na hivyo kurahishisha wanafunzi kupata masomo kwenye maeneo ya karibu.
‘Tuna kila sababu ya kumshukuru Mama Samia na kuendelea kusimama naye kwani ametufanyia mengi sisi wananchi wa Kibiti. Licha ya kuwa na shule za sekondari kwa kila kata, Mama Samia pia ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha VETA hapa wilayani na ujenzi huo tayari umeanza’, alisema Mpendu huku akisema hatua hivyo itawafanya wilaya kuendelea kusonga mbele kimaendeleo kwani Vijana watakuwa na ujuzi wa kujiajiri mara baada ya kukamilisha mafunzo yao.
Katika hatua nyingine, CCM imejipange kutumia michezo kama moja ya njia ya kuhamashisha wananchi kushiriki uchanguzi wa serikali za mitaa 2024 pamoja na kuendelea kutangaza mafanikio ya chama kwa miaka mitano iliyopita.
Mratibu na mdau wa mpira wa miguu nchini na mratibu wa michuano ya Ndondo Cup Shafih Dauda amesema kuwa kwa mwaka huu, mashindano hayo yatachezwa wilayani hapo na atashirikiana na CCM wilaya kuhakikisha kuwa wanatumia hiyo fursa kuhamashisha ushiriki wa uchanguzi wa serikali ya mitaa 2024 pamoja na kutengeneza mafanikio ya chama kwa miaka mitano iliyopita.
‘Michezo kwa sasa ni Ajira, lakini pia ni moja kati ya michezo ambayo inapendwa sana hapa nchini kwetu. Kwa mwaka huu, watu wa Kibiti tunawaletea burundani ya Ndondo Cup na naomba kutoa wito huu mjitokeze kwa wingi kwani pia mtaweza kufahamu ni kwa namna ngani CCM imeweza kuwaletea mafanikio na pia malengo yao kwenye kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa’, alisema Dauda.
Wilaya ya Kibiti inaundwa na kata 16 ambazo zote kwa sasa zinaongozwa na madiwani wa CCM. Kati hizo ni Bungu, Kibiti, Mjawa, Maparoni, Kiongoroni, Dimani, Mtawanya, Mlanzi, Salale, Msala, Mbuchi, Mahege, Mtunda, Mchukwi, Ruaruke na Mwambao.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Juma Kassim Ndaruke akimkabidhi cheti kama ishara ya kutambua kazi yake Mwenyekiti wa kijiji cha Mangombera kata ya Bungu wakati wa kikao cha madiwani wa wilaya ya Kibiti pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kilichofanyika Kibiti mwishoni mwa wiki. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kutoa tathmini ya utendaji kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwa miaka mitano iliyopita huku pia wakitengeza mpango kazi wakati huu wa kuelekea kwenye uchanguzi wa serikali za mitaa 2024.
Baadhi ya cha madiwani wa wilaya ya Kibiti pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wakishangilia hotuba ya mwenyekiti wao wa Wilaya ya Kibiti Juma Kassim Ndaruke wakati wa kikao cha madiwani wa wilaya ya Kibiti pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kilichofanyika Kibiti mwishoni mwa wiki. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kutoa tathmini ya utendaji kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwa miaka mitano iliyopita huku pia wakitengeza mpango kazi wakati huu wa kuelekea kwenye uchanguzi wa serikali za mitaa 2024.
Madiwani wa wilaya ya Kibiti pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mwenyekiti wao wa Wilaya ya Kibiti Juma Kassim Ndaruke wakati wa kikao cha madiwani wa wilaya ya Kibiti pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kilichofanyika Kibiti mwishoni mwa wiki. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kutoa tathmini ya utendaji kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwa miaka mitano iliyopita huku pia wakitengeza mpango kazi wakati huu wa kuelekea kwenye uchanguzi wa serikali za mitaa 2024. (Picha zote kwa hisani ya CCM Wilaya ya Kibiti)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment