Monday, July 1, 2024
Home
SPORTS
Serikali ya Marekani yashiriki Uzinduzi wa Ndondo Cup 2024, kupitia kampeni za SITETEREKI na FURAHA YANGU na CHANJO NI MAISHA
Serikali ya Marekani yashiriki Uzinduzi wa Ndondo Cup 2024, kupitia kampeni za SITETEREKI na FURAHA YANGU na CHANJO NI MAISHA
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam akipata vipimo vya afya wakati wa hafla ya uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup 2024. Serikali ya Marekani, kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) nchini Tanzania, imetangaza ushirikiano na
mashindano ya Ndondo Cup 2024 kupitia kampeni zake mashuhuri za
‘SITETEREKI’, ‘FURAHA YANGU’ na ‘CHANJO NI MAISHA’ ili kuchochea huduma
za VVU na chanjo. Mashindano haya yatafanyika katika mikoa nane nchini
Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma,
Pwani na Kagera.
Mashabiki wa mpira wa miguu kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup
2024. Serikali ya Marekani, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi
ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) nchini
Tanzania, imetangaza ushirikiano na mashindano ya Ndondo Cup 2024
kupitia kampeni zake mashuhuri za ‘SITETEREKI’, ‘FURAHA YANGU’ na
‘CHANJO NI MAISHA’ ili kuchochea huduma za VVU na chanjo. Mashindano
haya yatafanyika katika mikoa nane nchini Tanzania, ikiwemo Dar es
Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Pwani na Kagera.
Bi. Evangelina Chihoma ambaye ni Mtaalamu wa taarifa za
mkakati kutoka PEPFAR, akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano ya
Ndondo Cup 2024. Serikali ya Marekani, kwa kushirikiana na Wizara ya
Afya na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
nchini Tanzania, imetangaza ushirikiano na mashindano ya Ndondo Cup
2024 kupitia kampeni zake mashuhuri za ‘SITETEREKI’, ‘FURAHA YANGU’ na
‘CHANJO NI MAISHA’ ili kuchochea huduma za VVU na chanjo. Mashindano
haya yatafanyika katika mikoa nane nchini Tanzania, ikiwemo Dar es
Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Pwani na Kagera.
WIZARA ya Afya, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Serikali ya
Marekani ( USAID na PEPFAR) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION,
wameungana na kamati ya maandalizi ya Ndondo Cup, na wadhamini wengineo
ikiwemo CRDB na ASAS, kusogeza huduma za afya hasa huduma za VVU na
chanjo. Ushiriki huu kwenye Ndondo Cup 2024, unafanywa kupitia kampeni
ya afya ya vijana iitwayo SITETEREKI, kampeni ya wanaume kupambana na
VVU iitwayo FURAHA YANGU na Kampeni yab chanjo ya kitaifa iitwayo CHANJO
NI MAISHA. Mashindano ya Ndondo Cup 2024 yatafanyika katika mikoa nane
ya Tanzania - Dar es Salaam, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Kagera, Dodoma,
Mwanza, na Pwani.
Mashindano
yalianza rasmi Juni 30, 2024, na mechi ya ufunguzi ya kusisimua kati ya
Manzese Warriors na Makuburi FC kwenye Uwanja wa Kinesi, kata ya Sinza.
Washiriki walipata huduma kamili za afya, ikiwa pamoja na vipimo vya
VVU na matibabu na huduma za chanjo. Mgeni rasmi aliyefurahishwa na
mpango huu wa ubunifu, aliipongeza kamati ya maandalizi na wadhamini kwa
kujumuisha burudani na huduma za afya.
"Tumejitolea kubuni mbinu zinazotoa matokeo halisi ya kiafya," alisema Evangelina Chihoma kutoka Ofisi ya PEPFAR.
"Tunaamini
kwamba michezo inaweza kuongeza nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko ya
tabia na kuboresha upatikanaji wa huduma, na tunafurahia kushirikiana
na Ndondo Cup na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanikisha
mashindano haya."
Lulu Msangi, Mtaalamu wa
Programu kutoka Shirika la maendeleo la Marekani (USAID) aliongezea,
"Tunatumia michezo kuhamasisha Watanzania kupata chanjo na kulinda
familia zao."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment