ZANTEL YABORESHA MTANDAO WAKE KWA HUDUMA BORA ZAIDI - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, October 26, 2016

ZANTEL YABORESHA MTANDAO WAKE KWA HUDUMA BORA ZAIDI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ZANTEL YABORESHA MTANDAO WAKE KWA HUDUMA BORA ZAIDI

·         Wateja kuseti simu zao kwenye “automatiki” kuwawezesha kupata  mawasiliano ya uhakika mahali popote.

Dar es Salaam, Ijumaa 21 Oktoba  2016.  Katika kuhakikisha wateja wake wanapata mawasiliano ya uhakika, Zantel ipo mstari wa mbele katika kufanya  maboresho katika mtandao wake ili kuhakikisha kila mmoja anafurahia huduma na bidhaa zao mbalimbali ikiwemo kasi ya mtandao wa 4G.

 Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin anasema, “Tumeendelea kuwekeza katika mtandao wetu kuhakikisha kila mmoja Tanzania anafurahia manufaa ya teknolojia ya simu za mkononi ya Zantel. Uboreshaji huu unaoendelea utaimarisha ubora wa mtandao wetu, kuwa na mtandao ulioenea zaidi kuliko yote hapa nchini na kuwezesha upatikanaji wa intaneti ya kasi kupitia mtandao mpya wa 4G.    


Kutokana na mchakato kiufundi kwatika uboreshaji wa mtandao, wateja wa Zantel  watahitajika kuhakikisha simu zao zimerekebishwa mpangilio (setting) kuwa atomatik. Zoezi ambalo linaanza sasa mpaka Desemba 31, 2016.

 Kwa ajili hiyo tunawaomba wateja wetu kurekebisha simu zao na kuziweka katika sehemu inayoruhusu yenyewe uchaguzi wa mtandao  Automatic Network Selection” kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano ya inteneti ili waendelee kufurahia huduma bora za Zantel.


“Tumejizatiti kuhakikisha mtandao wetu unatoa huduma bora endelevu kwa matarajio ya wateja wetu, wamiliki na wadau wengine muhimu. Kupitia mipango tuliojiwekea, na uwekezaji katika miundo mbinu yetu, tumechukua hatua za makusudi kuhakikisha wateja wetu katika kila kona ya nchi  hawachwi nyuma na  mageuzi haya ya kiteknolojia”, aliongeza.   

Mtandao wa kisasa wa Zantel ulioboreshwa utawawezesha wateja kupata mawasiliano bora na yenye kasi katika upatikaji wa inteneti. Nchi pia itanufaika kwani kasi ya inayopatikana katika mtandao wa 4G itaziwezesha biashara na maendeleo ya teknolojia ya ubunifu na huduma za kidigitali.  

Zantel inawakaribisha kila mmoja kujaribu na kufurahia intaneti ya kasi ya 4G.

MWISHO.

Kwa taarifa zaidi kuhusu Zantel tembelea; www.zantel.com

Rukia Mtingwa – Brand and Communication Manager

Simu: +255 774 55 9999


Notes to the Editor:

Zantel believes that apart from offering a solid platform of technological innovation, sustainable investment is the bedrock of stellar growth and economic stability. Zantel consistently demonstrates its core values of affordable, consistent and seamless services through its International Gateway services, Fixed, Mobile, data services through its 4G and 3G networks and mobile Finance services popularly known as ‘Ezypesa”. 

Zantel is one of Millicom’s brands. Millicom is a leading telecom and media company dedicated to emerging markets in Latin America and Africa. Millicom sets the pace when it comes to providing innovative and customer-centric digital life style services to the world’s emerging markets.

The Millicom Group employs more than 16,000 people and provides mobile services to over 62 million customers. Founded in 1990, Millicom International Cellular SA is headquartered in Luxembourg and listed on NASDAQ OMX Stockholm under the symbol MIC.

No comments:

Post a Comment

Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar

Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...

Pages