Wednesday, March 27, 2019
Kampuni ya usafirishaji abiria mtandaoni ya Little yazinduliwa
Meneja Mkuu wa Huduma wa kampuni ya usafiri ya Little akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana.
Kutoka kulia ni Jefferson Aluda Meneja Huduma, Meneja Mkuu wa Huduma wa kampuni ya usafiri ya Little na Abbas Mfundo Mkurugenzi Mtendaji wakipiga makofi mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri jijini Dar es salaam jana.
Jefferson Aluda Meneja Huduma Kampuni ya Little akizungumz katika uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau walioalikwa kwenye uzinduzi huo wakiwa katika picha ya pamoja.‘
Meneja Masoko wa kampuni hiyo Bw. Katimpu Kisessa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo.
Wadau kutoka DSTV kushoto ni Grace Mgaya na Katibu Muhtasi Levina Bandiai wakiwa katika uzinduzi huo.
Hussein Machozi na bendi yake akitumbuiza katika hafla ya uzinduzi huo
Picha mbalimbali zikionyesha wadau waliohudhuria katika hafla hiyo katika uzinduzi huo.
KAMPUNI ya usafirishaji abiria mtandaoni ya Little imezindua huduma ya usafiri kwa Jiji la Dar es Salaam huku ikisema wao wamekuja tofauti na kampuni nyingine zinazoto huduma hiyo na hivyo watakaotumia usafiri wa Little watafurahia huduma bora na nzuri.
Katika kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kila mahali tayari Kampuni ya Little imeshasajili zaidi ya madereva 500 ambapo pamoja na mambo mengine wamehakikishiwa usalama wao ikiwemo kuwa na bima ya afya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana usiku wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo ,mmoja wa Wkurugenzi wa Little nchini Tanzania Abbass Mfundo amesema kabla ya kuanzisha huduma hiyo wameangalia changamoto zilizoko kwenye kampuni nyingi zinazotoa huduma ya kusafirisha abiri na kisha wao kuja tofauti kabisa jambo ambalo linawapa matumaini huduma zao zitakuwa bora.
Amesema kwa watakaotumia usafiri wa Little kuna huduma nne muhimu ambazo watazipata wakiwa safarini.Ametaja huduma hizo ni mteja kuona gharama ya safari yake kila baada ya dakika mbili na hivyo itamuwezesha kujua gharama kadri safiri inavyoendelea.
Amesema kumuwepo na kawaida ya baadhi ya abiria wasiokuwa waamini kuwaonesha abiria wao bei ambayo ni tofauti.”Kuna baadhi ya madereva wana Screen Short bei na kisha anamuonesha mteja huku akijua sio ya wakati huo.Hivyo kwetu dereva hawezi kuonesha bei tofauti na ile halisi kulingana na safari husika,”amesema Mfundo.
Pia amesema kutakuwa na huduma ya kumuwesesha abiria akiwa safarini mwingine anayetaka kujua atafahamu alipo kupitia ‘Safari share’ ambapo ametoa mfano ukiwa safarini mhusika atamuunganisha mtu wake na kisha atakuwa anajua mahali alipo.
Ameongeza huduma nyingine ambayo ni muhimu sana abiria au dereva wanapokuwa na mashaka kila mmoja kwa wakati wake ataweza kutoa taarifa kwa kubonyeza kitufe cha ‘Panic’ ambacho kitatoa taarifa katika kampuni ya ulinzi ambayo Little imeingia nayo mkataba.
Amesema wamefanya hivyo ili kuhakikisha wanaotumia usafiro huo iwe kwa dereva au abiria wote wanakuwa salama na kwamba kupitia huduma hiyo ni rahisi kupata msaada na kama kulikuwa na tatizo la tishio la usalama basi litakuwa limepata ufumbuzi wake.
Wakati huduma nyingine ambayo inapatikana Little na kwingine hakuna ni abiria(mteja) kuwa na uwezo wa kuchagua dereva anayemuhitija kwani kupitia App yao kuna sehemu ambayo utaona picha ya dereva na namba yake ya simu,hivyo kama alikupakia kwa mara ya kwanza na huduma yake ukaifurahia unaweza kumuita tena na kama hukuridhika naye unamkataa.
Pia amesema kwa kampuni ya Little wamekuwa wakisikia malalamiko ya madereva na hasa kuchelewa kulipwa fedha zao kwa wateja wanaotumia kadi,hivyo kwao hata kama dereva atampakia mteja anayelipa kwa kadi hata ikiwa kwa wiki,dereva atalipwa fedha yake siku hiyo hiyo.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Little Katimpu Kisessa amesema katika kuhakikisha pande zote zinanuifa,kampuni yao imeamua kuweka mifumo itakayomuwezesha dereva aliyekuwa kwao kunufaika na kazi anayoifanya.
Amesema mbali ya Little kutoa ajira kwa watanzania wengi kutokana na kuanzishwa kwa huduma hiyo ya usafirishaji,pia wamezingatia usalama wa afya zao na ndio maana mbali ya kupata fedha kutokana na kazi hiyo wamezingatia umuhimu wa madereva kuwa na bima ya afya.
Kuhusu huduma ya Little amesema kwa sasa wameanza na Dar es Salaam na baadae itafuata Dodoma,Mwanza,Mbeya na Arusha huku akisisitiza kuwa Little imekuja kivingine na kwamba huduma ambazo wao wanazo haziko kwenye kampuni nyingine.
“Little hatutaki ujanja ujanja kama ambao unafanywa na wengine.Ndio maana baada ya kupakua App yetu mteja kwa maana ya abiria kila kitu ataona kwenye simu yake ya mkononi.Kuna ile tabia inayoitwa kuchezesha dishi kwa kuonesha nauli ambayo sio ya kweli,huku kwetu hakuna.Ukitaka ku-screen short nauli itakukatalia,” amesema Kisessa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment