Thursday, August 8, 2019
DCB KUSHIRIKIANA NA MANISPAA KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT), uliofanyika mjini Mwanza hivi karibuni. Katikati ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo. (Picha na DCB).
Wziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa baada ya kukabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa (hayupo pichani), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Serikali
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Baisahara ya DCB imesema itaendelea kushirikiana kwa karibu zaidi na manispaa mbalimbali nchini na kwa sasa ikija na mpango maalumu kupitia huduma maalumu (municipal bonds), ili kuziwezesha manispaa hizo kupata pesa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati.
Akizungumza Jijini Mwanza hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema mpango huo utakaosaidia upatikaji wa fedha kuendesha miradi ya kimkakati una masharti wezeshi kwa mkopaji na tayari wameshaanza mazungumzo na manispaa na wadau wengine muhimu katika mchakato huo.c
"Mchakato wa uanzishwaji wa huduma hii unaendelea tutakachofanya ni kuongeza manispaa na halmashauri nyingine ambazo pia zina miradi ya kimkakati kuweza kujumuishwa kwenye mpango huu.
“Ombi langu ni kwamba najua vyanzo viko vingi lakini hii yenyewe inaweza ikawa chanzo kizuri cha kutafuta pesa, na vilevile ni chanzo kizuri kwa ajili ya kusaidia umma wa wawekezaji wakubwa na wadogo kupata fursa ya kuwekeza kwenye miradi yetu”, aliongeza.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa DCB alizungumzia pia udhamini na ushiriki wao katika mikutano mbalimbali na shughuli za kijamii ikiwemo Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT) uliofanyika mjini Mwanza hivi karibuni akisema hiyo imetokana na azma ya kuanzishwa kwa benki hiyo ikiwa na kuwahudumia wananchi na wajasiriamali wadogowadogo hasa wanawake na vijana na kufanikiwa kwa azma hiyo kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano kutoka katika manispaa na halmashari za Jiji la Dar es Salaam ilikoanzishwa.
"Tumekuwa tukishirikiana kwa karibu sana na manispaa na halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam katika kutoa mikopo ya wanawake na vijana na mafanikio ni makubwa mpaka sasa hivi ukiaangalia hiyo pesa iliyotoka na wanufaika wamenufaika mara tatu na hii ni kwa sababu ya weledi na uzoefu tulionao”, alisema.
Akizungumza mafanikio ya zoezi la uuzaji hisa lililofanyika hivi karibuni Bwana Ndalahwa alisema zoezi hilo lilifanikiwa kwa asilimia 108 na hiyo imechangiwa sana na historia yao na mahusiano yao ya karibu na manispaa na halmashauri kwa maana ya kwamba wao ndiyo waanzilishi.
Kuhusu maendeleo ya DCB na mikakati ya kuzidi kujipanua, Mkurugenzi wa DCB alisema wigo wa kufanya biashara umeongezeka kutoka Dar es Salaam pekee na sasa wameruhusiwa kuendesha biashara nchini nzima wakiwa na matawi manane likiwemo la Dodoma pamoja na mawakala 1000 nchi nzima huku wakipatikana kwenye mtandao hivyo huduma zao kupatikana nchi nzima.
Pamoja na hayo mkurugenzi hiyo alizungumzia huduma yao mpya ya DCB Lamba kwanza inayomwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 siku mteja anapoamua kuwekeza huku akitoa wito kwa watanzania kujiunga na huduma ya DCB Digital kwa njia ya simu za mkononi kwa kubonyeza alama ya nyota 150 nyota 85 reli ili kujiunga na kupata huduma mbalimbali za benki hiyo kwa lugha rahisi wakiita ‘DCB kwanza simu yako Tawi letu’.
Benki ya DCB ilianzishwa mwaka 2002, ikianzishwa na Maspaa za Dar es Salaam na kujulikana kama Benki ya Wananchi wa Dar es Salaam. Lengo kuu ilikuwa ni kusaidia wajasiriamali wadogowadogo. Baada ya kuanzishwa iliweza kutekeleza lengo hilo na na kuendelea kukua. Mwaka 2008 ilikuwa benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), na iliendelea kukua hivyo hivyo na baadae kubadilisha jina kutoka Dar es Salaam Community Bank na kuwa DCB Commercial Bank kwa sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu y...
No comments:
Post a Comment