Wednesday, December 18, 2024
Home
BUSINESS
Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari
Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu ya Kampeni ya "Spend and Win" na hafla ya kukabidhi Subaru Forester kwa mshindi wa pili, Bi. Alyshah Bharwani (wa tatu kushoto), katika hafla jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Masoko wa Absa, Beda Buswalo. Mteja wa benki hiyo, Bi. Amalia Lui Shio, alitangazwa mshindi wa tatu.
Mshindi wa pili wa Kampeni ya "Spend and Win" ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Alyshah Bharwani (wa tatu kushoto), akionesha funguo za Subaru Forester mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), katika hafla jijini Dar es Salaam leo. Tukio hilo pia lilihusisha droo ya tatu ya kampeni, ambapo mteja wa benki hiyo, Bi. Amalia Lui Shio, alitangazwa mshindi. Kulia ni Bw. Jamil Kanji, mmoja wa wanafamilia wa Alyshah.
Benki ya Absa Tanzania imehitimisha rasmi Kampeni yake ya "Spend & Win" kwa mafanikio makubwa, kupitia droo ya tatu na ya mwisho iliyofanyika leo, ambayo imeashiria mwisho wa miezi mitatu ya msisimko, ubunifu, na zawadi kwa wateja.
Hafla hiyo ilipambwa na kutangazwa kwa mshindi wa tatu na wa mwisho, Bi. Amalia Lui Shio, ambaye atapokea zawadi yake—Subaru Forester ya mwaka 2014, Januari 2025.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ndabu Swere, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja Binafsi katika Benki ya Absa Tanzania, alimtangaza mshindi na kuwapongeza washindi wote watatu waliotangazwa katika kampeni hiyo.
'“Tunayo furaha kumtangaza Bi. Amalia Lui Shio kama mshindi wa droo ya tatu na ya mwisho ya Kampeni ya ‘Spend & Win’,” alisema Bi. Swere. “Stori yako ni muhimu, na kupitia kampeni hii, tumepata fursa ya kuwawezesha wateja wetu kubadilisha maisha yao. Bi. Amalia Lui Shio atapokea rasmi gari lake mwezi ujao, na tunasubiri kwa shauku kusherehekea tukio hili la kusisimua pamoja naye.”
Wakati wa hafla hiyo, Bi. Ndabu pia alikabidhi funguo za Subaru Forester ya mwaka 2014 kwa mshindi wa pili, Bi. Alyshah Aminmohamed Bharwani, ambaye alitoa shukrani za dhati kwa Benki ya Absa kwa zawadi hiyo ya kubadilisha maisha.
“Ninawashukuru sana Benki ya Absa kwa kampeni hii. Kushinda gari hili ni jambo kubwa sana kwangu na familia yangu, na nimefurahi sana kuwa sehemu ya safari hii,” alisema Bi. Bharwani.
Kampeni ya "Spend & Win" ambayo ilizinduliwa tarehe 10 Septemba 2024, iliwapa wateja wa Benki ya Absa Tanzania fursa ya kushinda moja kati ya magari matatu ya Subaru Forester kwa kufanya miamala kwa kutumia kadi zao za Absa au majukwaa ya kidijitali. Wateja walikidhi vigezo vya kuingia kwenye droo kwa kufanya angalau miamala 20 ya kadi yenye jumla ya TZS milioni 5 au zaidi kwa mwezi, huku miamala ya kidijitali ikiongeza nafasi zao za kushinda.
Akiongelea mafanikio ya kampeni hiyo, Bi. Ndabu aliwashukuru wateja wote waliopata nafasi ya kushiriki na kusisitiza dhamira ya benki hiyo ya kutoa suluhisho za kibunifu na uzoefu mzuri kwa wateja wake.
“Kwa niaba ya Benki ya Absa Tanzania, napenda kuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki kampeni hii na kuwapongeza washindi wetu watatu: Bw. Rashid Nassoro Said, Bi. Alyshah Aminmohamed Bharwani, na Bi. Amalia Lui Shio,” alisema Bi. Ndabu. “Katika Absa, tumejizatiti kuwawezesha wateja wetu na jamii, na kampeni kama hii ni mojawapo ya njia tunazotumia kuonyesha shukrani zetu huku tukitimiza dhamira yetu ya ‘Kuiwezesha Kesho Afrika ya kesho, Pamoja, Hatua moja baada ya nyingine."
“Tunapohitimisha kampeni hii, nataka kuwahakikishia wateja wetu kuwa huu sio mwisho. Absa itaendelea kuanzisha kampeni na fursa za kusisimua za kuwazawadia na kuwaunga mkono wateja wetu wanapofanikisha malengo yao.”
Hitimisho la Kampeni ya "Spend & Win" linaimarisha nafasi ya Benki ya Absa Tanzania kama benki ya kidijitali inayoongoza na mshirika wa kuaminika katika safari za kifedha za wateja wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu y...
No comments:
Post a Comment