Monday, August 12, 2019
MKUTANO WA KIKANDA WA KUPAMBANA NA MARADHI YA VIKOPE (TRACHOMA) WAFANYIKA ZANZIBAR
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said Suleiman akifungua
Mkutano wa siku mbili wa kupambana na maradhi ya vikope (Trachoma) Duniani kwa
nchi za Afrika Mashariki na Kati, mkutano huo umefanyika Hoteli Sea Cliff
Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
Baadhi ya wajumbe wa
Mkutano wa kumbambana na maradhi ya vikope Duniani wakisikiliza hutubaya ya
Naibu Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano huo.
Mkurugenzi mradi wa kupambana na maradhi ya vikope Duniani ,
Paul Emerson, akielezea juu ya juhudidi zinazochukuliwa kuhakikisha maradhi ya
vikope yanaondoka duniani kote.
Msaidizi Meneja Kitengo cha Maradhi yasiyopewa kipaumbele Salum
Abubakar (alieshika maiki) akijibu maswali ya wajumbe wa mkutano huo mara
baada ya kuwasilisha mada ya uzoefu wa Zanzibar kama kisiwa katika kupambana na
maradhi ya vikope.
Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed
Abdalla(kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi mradi wa kupambana na
maradhi ya vikope Duniani, Paul Emerson.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Afya Zanzibar Harusi Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
mkutano wa kupambana na maradhi ya vikope (Trachoma) uliofanyika Hoteli ya Sea
Cliff Mangapwani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu y...
No comments:
Post a Comment