MAMBO MATATU MUHIMU YATAJWA MIAKA MITANO YA M-PAWA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, July 18, 2019

MAMBO MATATU MUHIMU YATAJWA MIAKA MITANO YA M-PAWA


Benki ya CBA ikishirikiana na kampuni ya Vodacom imefanya droo yake ya 5 ya kuadhimisha miaka 5 ya huduma ya MPawa yenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa wateja wake kwenye makao makuu ya benki hiyo Dar es salaam. 

Katika kusherehekea maadhimisho hayo, promosheni hiyo inajumuisha droo za kila wiki zilizohusu kuwekeza na kukopa na MPawa huku ukitoa washindi zaidi ya 340 walioibuka na mara mbili ya akiba zao kuanzia kiwango cha Tsh 1000-200,000, simu janja na muda wa maongezi.


Katika kuongelea kuhusu huduma hii ya MPawa, Meneja Masoko wa benki hiyo Bw Solomon Kawiche aligusia mambo 3 muhimu kwenye maadhimisho hayo. 


M-Pawa inasherehekea miaka 5, ni mafanikio gani yameonekana tangu kuanzishwa kwa huduma hii? Mpawa ilianza na wateja 4 tu ila hadi leo hii imefikisha wateja Mil 8.5 na imefanikiwa kurahisisha Maisha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki kwa kuwapatia huduma nafuu.


Ikiwemo kukopa kiasi kidogo cha hadi 1000 ambacho hauwezi kupata kupitia huduma za benki. M-Pawa imefanikiwa kutoa huduma ya kuhifadhi akiba kwa kiwango cha chini cha hadi Tsh 1, hakuna benki nyingine ndani ya Tanzania inayotoa huduma kama hii na kurahisisha huduma za kibenki bila ya kuwa na
utaratibu mrefu kukamilisha miamala.

kupitia huduma hii, wateja wetu wanapata faida kupitia akiba zao. Akiba za wateja wa MPawa pia zipo kwenye usalama wa hali ya juu kwasababu hakuna makato wala gharama zilizofichika.

MPawa imeinua hali ya Maisha ya mamilioni ya watanzania hususani wafanyabiashara wadogo na bila kusahau kuwa imekuwa ikitoa uhakika wa kifedha wakati wa dharura; mteja anaweza kukopa muda wowote na wakati wowote ule.

Nini malengo ya baadae ya M-Pawa?

Ikiwa ni huduma ya kwanza ya kidigitali Tanzania, MPawa itaendelea kugusa miasha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki na itaendelea kujidhatiti kwenye kuwajumuisha kifedha wateja wake.

Kama benki, tuna maleno ya kuwekeza zaidi kwenye huduma hii kuhakikisha kuwa inaendana na maendeleo ya sasa ya kisayansi na Teknolojia na kuwezesha huduma hii kwenye application.

Nini maoni yako kwenye huduma za kifedha za kiditali hususani M-Pawa?

Huduma za kifedha za kidigitali kwenye dunia ya leo ni sio kitu ya kupuuza hususani huduma kama



MPawa inapatika kupitia simu yoyote ya mkononi, ni huduma ya kibenki iliyorahisishwa kutumia mahalipopote kwa gharama nafuu na humpatia mteja faida kupitia akiba anayoweka bila kuwa na gharama zilizofichwa.

Hili linaupa upekee huduma hii ya M-Pawa Mshindi mkubwa wa maadhimisho haya ya Miaka 5 ya MPawa ataibuka na zawadi ya Million 15 za kitanzania kwenye droo ya mwisho ya promosheni hiyo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii, wateja wanaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya benki ya



1 comment:

Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu y...

Pages